Makazi ya Far West, Missouri, yalikuja kuwa makazi kwa Watakatifu 3,000 hadi 5000 waliotafuta kimbilio kutokana na mateso katika Wilaya za Jackson na Clay. Mnamo mwaka 1838 Bwana aliwaamuru Watakatifu kujenga hekalu hapa (ona M&M 115:7–8) Mateso waliyofanyiwa na kundi la waovu yaliwazuia wao kufanya hivyo. Mnamo 31 Oktoba ya mwaka huo, Joseph Smith Nabii na viongozi wengine wa Kanisa waliwekwa rumande na, baada ya kusikilizwa mashtaka katika Richmond, wakafungwa gerezani la Liberty. Wakati wa majira ya baridi ya mwaka 1838–1839, Watakatifu wa Siku za Mwisho walifukuzwa kutoka Far West na maeneo mengine katika Missouri na wakahamia makao mapya katika Ilinois.