18. Hekalu la Salt Lake
Hekalu la Salt Lake likiangaliwa kutoka kaskazini mashariki. Siku chache baada ya kikundi cha kwanza cha payonia cha Watakatifu wa Siku za Mwisho kuingia katika Bonde la Salt Lake, Rais Brigham Young alichoma ardhi kwa fimbo yake ya kutembelea na kutamka “Hapa tutajenga hekalu la Mungu wetu.” Ardhi ilivunjwa 14 Februari 1853. Mnamo 6 Aprili 1853, mawe ya msingi yaliwekwa. Hekalu lilikamilika na kuwekwa wakfu miaka 40 baadaye 6 Aprili 1893. Urais wa kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili walikutana hapa kila wiki ili kutafakari kwa makini na kuomba mwongozo wa Bwana katika kuhudumu na kujenga ufalme wa Mungu.
Matukio muhimu: Bwana amewapa Marais wa Kanisa na Viongozi Wakuu wengine mbubujiko wa roho wa ufunuo hapa, ikiwa ni pamoja na Tamko Rasmi 2. Hivi karibuni zaidi, Urais wa Kwanza na Baraza la Mitume Kumi na Wawili kwa kauli moja waliidhinisha na kuchapisha “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Ibada za hekalu zinazofanyika kwa wazima na wafu zimebariki maishi ya mamilioni.