Misaada ya Kujifunza
2. Kilima Kumora na Eneo la Palmyra-Manchester


2. Kilima Kumora na Eneo la Palmyra-Manchester

picha 2

Ukiangalia kuelekea kaskazini, picha hii inaonyesha Kilima Kumora katika Manchester, New York. Kilima kinaonekana katika kona ya chini ya mkono wa kulia wa picha na kinaendelea kidogo zaidi ya nusu kwa juu ya picha. Sanamu nyeupe inayoonekana upande wa kaskazini mwishoni mwa kilima ni kwa heshima ya malaika Moroni na kutokea kwa Kitabu cha Mormoni. Kilima Kumora kiko karibu kilomita zipatazo 5 kusini mashariki mwa Kijisitu Kitakatifu. Karibu na juu kabisa ya picha ni Palmyra, umbali wa kilomita 6½. Shamba la Smith na Kijisitu Kitakatifu vipo upande wa juu zaidi wa kushoto wa picha hii.

Matukio muhimu: Familia ya Nabii Joseph Smith iliishi katika eneo hili wakati wa Ono la Kwanza (JS—H 1:3). Katika mwaka 421 B.K., Moroni alizika seti ya mabamba ya dhahabu katika Kilima Kumora yaliyokuwa na historia takatifu ya watu wake (M. ya Morm. 1:1–11; Morm. 6:6; Moro. 10:1–2). Moroni huyu alimwambia Joseph Smith mahali pa kuyapata mabamba hayo pale kilimani. Moroni alimpa yeye katika mwaka wa 1827 (M&M 27:5; 128:20; JS—H 1:33–35, 51–54, 59).