Misaada ya Kujifunza
12. Gereza la Liberty


12. Gereza la Liberty

Picha
picha 12

Gereza Liberty, Missouri karibu mwaka 1838. Joseph Smith na viongozi wengi watano wa Kanisa waliwekwa gerezani ndani ya kuta zake nne za unene wa mita 1.2 (futi 4) tangu 1 Desemba 1838, hadi 6 Aprili 1839. (Sidney Rigdon aliachiwa huru mwishoni mwa Februari.) Wakiwa wamefungiwa chumba cha chini au gereza la chumba cha chini cha jengo hili, walilala juu ya mawe yenye baridi, sakafu iliyotawanywa na majani makavu na chenye mwanga mdogo na hifadhi haba dhidi ya majira ya baridi kali.

Tukio muhimu: Joseph Smith Nabii, akiomba kwa ajili ya maelfu ya Watakatifu wa Siku za Mwisho wakiwa wanafukuzwa kutoka Missouri, alipokea jibu la sala yake, ambalo aliliandika katika barua kwa Watakatifu waliokuwa uhamishoni (M&M 121–123).

Chapisha