Misaada ya Kujifunza
15. Hekalu la Nauvoo


15. Hekalu la Nauvoo

picha 15

Hekalu halisi lilijengwa kutokana na chokaa ya kijivu-nyeupe ya kutoka hapo. Jengo lilikuwa na vipimo vya mita 39 urefu na mita 27 upana. Kilele cha mnara kilisimama mita 48 juu ya usawa wa ardhi. Waumini wa Kanisa walifanya dhabihu kubwa kwa kujenga hekalu hili zuri, wakianza kazi katika mwaka 1841. Wengine walifanya kazi kwa miezi mingi katika jingo hili; wengine walitoa dhabihu ya fedha zao. Ingawa lilikuwa halijaisha kikamilifu, hekalu lilijaa kabisa wakati waumini wakija kwa ajili ya ibada kwa miezi kadhaa kabla ya kukimbilia Magharibi. Wakati Watakatifu wengi waliondoka Nauvoo mapema katika majira ya kuchipua ya mwaka 1846 kwa sababu ya vitisho vya ghasia za wahuni, kikosi maalumu kilibaki nyuma kumalizia hekalu. Mnamo 30 Aprili 1846, Mzee Orson Hyde na Wilford Woodruff wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na wengine wapatao 20 waliiweka wakfu nyumba hii ya Bwana. Hekalu lilihamwa mwezi Septemba wakati waumini wa Kanisa waliosalia walipofukuzwa Nauvoo; majeshi ya wahuni kisha wakalichafua jengo hili takatifu. Kwa ndanililiangamizwa kwa moto mwezi Oktoba 1848. Hekalu hili lililo jengwa upya (lililopigwa picha hapa), limejengwa kama lilivyokuwa mwanzoni, likawekwa wakfu na Rais Gordon B. Hinkley 27–30 Juni 2002.

Matukio muhimu: Mkutano Mkuu ulifanyika katika chumba cha mikutano cha hekalu 5 Oktoba 1845. Kazi ya Endaumenti ilianza mnamo 10 Desemba 1845 na kuendelea hadi 7 Februari 1846. Zaidi ya Watakatifu wa Siku za Mwisho 5500 walipokea endaumenti zao, na ubatizo mwingi kwa ajili ya wafu na kuunganishwa kwingi kulifanywa.