Misaada ya Kujifunza
6. Eneo la Nyumba ya Peter Whitmer Mkubwa


6. Eneo la Nyumba ya Peter Whitmer Mkubwa

Picha
picha 6

Nyumba hii ya magogoinawakilisha nyumba halisi ya Peter Whitmer Mkubwa katika Fayette, New York.

Matukio muhimu: Joseph Smith alimaliza tafsiri ya Kitabu cha Mormoni hapa katika mwishoni mwa Juni, 1829. Kichakani karibu na nyumba hii, wale Mashahidi Watatu walimwona malaika Moroni na yale mabamba ya dhahabu. Ushuhuda wao sasa umepigwa chapa katika nakala zote za Kitabu cha Mormoni. Mnamo 6 Aprili 1830, karibu watu 60 walikusanyika katika nyumba hii ya Peter Whitmer ili kushuhudia uanzishwaji rasmi wa Kanisa la Yesu Kristo (M&M 20). Mikutano ya kwanza ya Kanisa changa ilifanyika hapa. Ishirini kati ya mafunuo yaliyomo katika Mafundisho na Maagano yalipokelewa na Joseph Smith nyumbani mwa Peter Whitmer.

Chapisha