Salamu kutoka Mexico!
Ungana na Margo na Paolo wanaposafiri kuzunguka ulimwengu ili kujifunza kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni.
Mexico ni nchi iliyoko Amerika Kaskazini. Inakadiriwa kuwa na watu milioni 126.
Kitafunwa kitamu
Guacamole ni supu iliyotengenezwa kutokana na parachichi. Watu huila kwenye chapati yenye mchanganyiko wa vyakula, katika saladi au kwa chipsi za mahindi. ¡Deliciosoi!
Kukutana kwa Pamoja
Hili ni jengo la Kanisa la Mexico. Mexico ina karibu waumini wa Kanisa milioni 1.5—ya pili kwa nchi yoyote duniani!
Baile Folklórico (Ngoma ya Watu)
Sehemu nyingi za Mexico zina mitindo yao wenyewe ya muziki, dansi na mavazi. Msichana huyu amevaa mavazi ya watu kutoka Chiapas.
Tamaduni za Kale
Mexico ina majengo mengi yaliyotengenezwa na watu wa kale. Kila mwaka, mamilioni ya watu hutembelea piramidi hii ya Mayan huko Chichen Itza katika jimbo la Yucatán.
Mahekalu Mengi
Mexico ina mahekalu 13 yaliyowekwa wakfu, na mengine yapo njiani. Mvulana huyu alitembelea hekalu huko Veracruz.