2022
Magugu na Maneno Mabaya
Septemba/Oktoba 2022


Magugu na Maneno Mabaya

“Kwa nini tusiweke ahadi ya familia?” Mama aliuliza.

mom and boy weeding together

“Tunaweza kuzungumza?” Jonas alimuuliza Mama. Jonas aliketi kwenye nyasi karibu na mahali mama yake alipokuwa akipalilia maua.

“Hakika. Nini kinaendelea?” Mama aliuliza. Alivua glavu zake chafu za bustani.

“Leo shuleni baadhi ya watoto walikuwa wanasema neno nisilolijua. Walicheka walipolisema,” Jonas alisema. “Nadhani lilikuwa neno baya.”

“Ulihisi vipi uliposikia neno?” aliuliza Mama.

“Sikuhisi vizuri.”

Jonas alimnong’oneza mama neno hilo. Mama alimwambia maana yake. Jonas alikuwa sahihi. Halikuwa neno zuri.

“Lakini kwa nini ni baya?” Jonas aliuliza.

“Ni baya kwa sababu si jema na halina heshima. Tunapotumia maneno kama hayo, inakuwa vigumu kwa Roho Mtakatifu kuwa nasi. Roho Mtakatifu alikuwa akikuambia kwamba lilikuwa baya. Ndio maana hukuhisi vizuri.”

Jonas alikunja uso. “Lakini watoto wengine walionekana kuwa na furaha. Kwa nini mimi pekee ndiye niliyekuwa na wasiwasi?”

“Unajuaje kwamba watoto wengine hawakuhisi vivyo hivyo?” Mama aliuliza.

“Kwa sababu wote walicheka na kutabasamu mtu aliposema neno hilo.” Jonas alihisi kukanganyikiwa.

“Nyakati zingine watu hucheka au kutabasamu wanapohisi wasiwasi,” Mama alisema. “Na wakati mwingine wanaposikia au kusema maneno mabaya sana, haiwasumbui tena. Lakini bado si sahihi kusema maneno hayo. Ni kama magugu haya. Ninayang’oa ili kuweka bustani safi na kuruhusu mimea mizuri ikue.”

“Nimefurahi kwamba sikusema neno,” Jonas alisema.

“Mimi pia,” alisema Mama. “Najivunia kuwa nawe. Na nina wazo. Kwa nini tusiweke ahadi ya familia?”

“Ipi hiyo?” Jonas aliuliza.

“Tuahidi kutumia maneno mazuri na sio maneno mabaya. Inaweza kuwa ni agano la familia.”

Jonas alipenda wazo hilo. Yeye na Mama wakapeana mikono. Jonas alihisi vizuri kuhusu ahadi aliyofanya na Mama.

“Sasa vipi ukiniahidi kunisaidia kumalizia palizi?” Mama aliuliza. “Kisha nitakuahidi kukupeleka uwanja wa michezo.”

Jonas alitabasamu na kuokota jembe. “Nimekubali.”

Alipokuwa akimsaidia Mama, Jonas alihisi vizuri zaidi. Alijua kuahidi kutotumia maneno mabaya lilikuwa chaguo zuri kwa familia yao.

Kielelezo na Dan Widdowson