2022
Acha Mungu Ashinde!
Septemba/Oktoba 2022


Kutoka Urais wa Kwanza

Acha Mungu Ashinde!

Imetoholewa kutoka “Acha Mungu Ashinde,” Liahona Nov. 2020, 92–95.

Picha
boy and girl standing and looking happy

Je, unajua inamaanisha nini kumwacha Mungu ashinde? Inamaanisha kwamba tunamwacha Yeye awe ushawishi wenye nguvu zaidi katika maisha yetu.

Je, wewe uko radhi kuacha Mungu ashinde katika maisha yako? Je, utaruhusu neno Lake, amri Zake na maagano Yake, yaathiri kile unachofanya kila siku? Je, utairuhusu sauti Yake iwe muhimu zaidi kuliko nyingine yoyote?

Unaporuhusu Mungu ashinde, utajifunza kweli za milele ili kuongoza maisha yako. Unapomruhusu Mungu ashinde, chaguzi nyingi huwa rahisi. Utajua:

  • Kipi cha kuangalia na kusoma

  • Jinsi ya kutumia muda wako

  • Kipi unataka kufikia

  • Ni mtu wa aina gani wewe unataka kuwa

Inahitaji imani na ujasiri ili kuacha Mungu ashinde. Unavyomuacha ashinde, utajua kuwa Mungu wetu ni “Mungu wa miujiza” (Mormoni 9:11).

Ungefanya nini?

Picha
Page from the September/October 2022 Friend Magazine.

Je, ungesamehe?

sikukusudia.

Je, ungekuwa mwaminifu?

Je, nichukue?

Je, ungekuwa mwema?

Je, ungependa kuchagua kutazama kitu kizuri?

Inachekesha sana! Kila mtu anaongea hivyo.

Vielelezo na Kiersten Eagan

Chapisha