2022
Kutana na Jarom kutoka Mexico
Septemba/Oktoba 2022


Mikono ya Usaidizi Ulimwenguni Kote

Kutana na Jarom kutoka Mexico

Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.

boy in blue shirt

Yote kuhusu Jarom

boy holding up pets

Umri: miaka 10

Kutoka: Jiji la Mexico, Mexico

Lugha: Kihispania

Malengo na ndoto: 1) Kuwa daktari wa mifugo au mwanasaikolojia. 2) Kuchora picha nzuri. 3) Kuwatendea wengine kwa heshima na wema.

Familia: Jarom, Mama, Baba, kaka wawili

Mikono ya Kusaidia ya Jarom

boy taking care of dogs

Jaromu ana mbwa watatu. Moja ya kazi yake ni kuwalisha kila siku. Anawapenda sana. Jarom pia ni msikilizaji mzuri na mmisionari. Alipojua kwamba babu wa rafiki yake alifariki, Jarom alimwita rafiki yake. Jarom alimsikiliza rafikiye. Pia alimfariji na kumwambia kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu.

Jaromu anataka marafiki zake wawe na furaha. Mara nyingi anazungumza nao kuhusu Kanisa na kuwaalika kwenye mikutano na shughuli. “Unapoomba, kumbuka marafiki na familia yako,” Jarom anasema. “Uliza kujua jinsi unavyoweza kuwasaidia.”

Mambo Pendwa ya Jarom

illustrations of Jarom’s favorites

Sehemu: Hifadhini na kanisani

Hadithi kuhusu Yesu: Pale Yesu lipomsaidia kipofu na wakati alipofufuka.

Wimbo wa Msingi: “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103)

Vyakula: Supu ya pozole, chipsi na donati

Rangi: Bluu na zambarau

Masomo Shuleni: Historia na jiografia

Page from the September/October 2022 Friend Magazine.

Vielelezo na Mike Laughead