2022
Yesu Alituahidi Faraja
Septemba/Oktoba 2022


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Alituahidi Faraja

Picha
Jesus sitting with disciples

Yesu Kristo alijua kwamba wanafunzi Wake wangehitaji faraja baada ya Yeye kufa. Kwa hiyo aliwafundisha kuhusu Roho Mtakatifu. Aliahidi kwamba Roho Mtakatifu angewafariji na kuwa pamoja nao daima. Jina moja la Roho Mtakatifu ni Mfariji. Tunapokuwa na huzuni au hofu, Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kukumbuka upendo wa Yesu Kristo.

Picha
A photo of Brooklyn Dean

Mama yangu, baba, na mimi tulitoa blanketi kwa hospitali ya watoto. Wafanyakazi wa hospitali hiyo walisema blanketi hizo zingewasaidia watoto wasiogope tena. Ninafurahi kwamba blanketi zetu zitasaidia kuwachangamsha watoto na kuwafanya wafurahi. Ilinifanya nifurahi sana pia.

Brooklyn D., miaka 9, Texas, Marekani

Chapisha