2022
Mambo Madogo Huleta Tofauti
Septemba/Oktoba 2022


Imeandikwa na Wewe

Mambo Madogo Huleta Tofauti!

boy smiling

Mimi ndiye mfupi zaidi katika darasa langu. Wakati fulani natamani ningekuwa mrefu kama wanafunzi wenzangu. Lakini mama yangu ananiambia kwamba maadili yangu ni muhimu zaidi kuliko urefu wangu, na ninaweza kufanya mambo mengi ingawa mimi ni mdogo kuliko wanafunzi wenzangu.

Ninapopoteza kitu au ninapoogopa, ninaacha kile ninachofanya na kuomba. Baba wa Mbinguni hujibu sala zangu.

Ninawasaidia binamu zangu na watoto wengine kusoma hesabu, Kiingereza na kuandika. Ninasaidia kufanya kazi za nyumbani. Ninatunza wanyama wangu vipenzi. Mimi huchora michoro ya sanaa na kuandika barua kwa ajili ya wamisionari. Ninaponunua au kupata kitu kipya, ninashiriki na wengine. Ninapoona watu wenye uhitaji barabarani, mimi hutoa ninachoweza na ninawaombea kila siku.

Nilipokuwa mdogo, mama yangu alianza kunisomea. Tunasoma hadithi za Kitabu cha Mormoni, hadithi za Biblia na gazeti la Rafiki. Sasa, ingawa nina umri wa miaka tisa, bado mama ananisomea. Siwezi kulala isipokuwa mama yangu asome nami. Lakini sasa nyakati fulani za usiku namsomea Mama hadi analala.

Ninafanya mambo haya rahisi ingawa mimi ni mdogo. Ninajua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanapenda watoto wadogo. Najua Wananipenda. Nawapenda pia. Ndoto yangu ni kuwa mmisionari ili nifanye mambo madogo zaidi kuleta mabadiliko makubwa.

Vielelezo na Adam Koford