2022
Jiunge
Septemba 2022


“Jiunge,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Septemba 2022

Jiunge

Lindsey B.

15, Kentucky, Marekani

Picha
msichana

Picha na Christina Smith

Mimi umri wangu ni miaka 15, na niko katika mwaka wa pili katika shule ya upili. Ninacheza michezo mitatu: mpira wa kikapu, mpira wa wavu, na mpira wa laini. Maisha yangu yametawaliwa na michezo na familia.

Wakati wa UVIKO, pamoja na sintofahamu ya mwaka wa shule, niliamua kumtumainia Bwana kuwa anafahamu kilicho bora kwa kila mmoja. Shule yangu kwa kweli ilirejea kampasi, kitu ambacho kilikuwa bora sana kwangu mimi, kwa kuwa mimi siyo msomaji mzuri sana nje ya shule.

Shuleni kwangu kuna waumini watatu tu wa Kanisa. Ni vigumu kidogo kwani hata hawako darasani kwangu wala si kidato kimoja na mimi. Lakini hata kama marafiki zangu wengi sio Watakatifu wa Siku za Mwisho, ninaweza kuwapata wengine wenye viwango vizuri vya tabia. Inanisaidia mimi kuzungukwa na watu ambao hawaniangushi.

Kwa “Msikilize Yeye,” ninapenda kutumia muda pekee yangu na kusali na kuangalia maandiko kuhusu matatizo yangu. Kufanya hili kunanisaidia mimi kujua Bwana anataka nifanye nini katika hali niliyopo na kufikiria jinsi ambavyo Yeye angejisikia.

Chapisha