“Sehemu ya Burudani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.
Sehemu ya Burudani
Shiriki Michezo Yako ya Nje
Ni ipi baadhi ya michezo upendeleayo kucheza nje na marafiki zako au familia? Mpira wa mikono ragbi? Mbwa mjanja? Kujificha na kutafutana? Kamata Bendera? Hiyo ni michache tu ya michezo ya nje inayochezwa kote ulimwenguni, lakini tunajua iko mingi zaidi unayoweza kutuambia juu yake.
Tafadhali tutumie maelezo ya mchezo wako pendwa wa nje (pamoja na picha, kama inawezekana) kwenye ftsoy@ChurchofJesusChrist.org kabla ya Oktoba 1, 2022. Tutaikusanya na kutoa baadhi ya mawazo ili sisi sote tuweze kujifunza michezo zaidi.
Njia za Burudani za Kusoma Maandiko
Ili kubadilisha mambo, ungeweza kujaribu moja ya mapendekezo haya kwa ajili ya kusoma maandiko.
-
Fikiria juu ya mtu mmoja ama wawili ambao wanataabika na usome maandiko yanayohusiana na mahitaji yao.
-
Tengeneza mchezo au usome kitamthiliya hadithi uipendayo ya maandiko.
-
Pamoja na familia au marafiki, mpeane zamu ya kujirekodi wenyewe wakati mkisoma maandiko. Kisha zipeleke rekodi hizo kwa watu wengine usio waona mara kwa mara, kama wamisionari.
-
Tengeneza vikaragosi vya soksi na viweke kwenye maonyesho ya vikaragosi vya sura au hadithi kutoka kwenye maandiko.
-
Soma kwa pamoja kwa njia ya video au kwa njia ya kumpigia mtu simu.
-
Kama unajifunza lugha nyingine, jaribu kusoma maandiko katika lugha hiyo na kisha itafsiri katika lugha yako.
-
Angalia video za maandiko kutoka Maktaba ya Injili (chini ya Videos na Images). Kisha soma vipengele au milango ambayo inafanana na video hizo.
Mzingile wa Nusu Dunia
Majani yanaanguka upande wa kaskazini mwa dunia wakati maua yanachanua upande wa kusini mwa dunia. Tafuta njia kutoka jani jekundu kileleni kwenda kwenye jani la njano chini. Unaweza kuruka kushoto, kulia, au chini (siyo kimshazari) kati ya alama ambazo ni za umbile moja au rangi. Mifano miwili ya miondoko imeonyeshwa. Kuna zaidi ya njia moja ya kukamilisha mzingile huu.