2022
Jifunze juu ya Yesu Kristo na Uzifikie Nguvu Zake
Septemba 2022


“Jifunze juu ya Yesu Kristo na Uzifikie Nguvu Zake,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Sept. 2022.

Neno la Mwisho

Jifunze juu ya Yesu Kristo na Uzifikie Nguvu Zake

Ningependa nishiriki nanyi jinsi tunavyoweza kuchota na kuingiza katika maisha yetu nguvu za Bwana wetu na Mwalimu, Yesu Kristo.

Tunaanza kwa kujifunza kumhusu Yeye.1 “Ni vigumu kwetu [sisi] kuokolewa katika ujinga” (Mafundisho na Maagano 131:6). Kadiri tunavyomwelewa mafundisho ya Mwokozi na kile alichofanya kwa ajili yetu sisi, ndivyo tunavyojua kwamba Yeye anaweza kutoa nguvu ambayo tunaihitaji kwa ajili ya maisha yetu.

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaitaja huduma Yake kama Upatanisho wa Yesu Kristo, ambao ulifanya ufufuko kuwa kitu halisi kwa ajili ya wote na umefanya uzima wa milele uwezekane kwa wale wanaotubu dhambi zao na kupokea na kushika ibada na maagano muhimu.

Chini ya mpango mkuu wa milele wa Baba, ni Mwokozi ndiye aliyeteseka. Ni Mwokozi ndiye aliyekata kamba za kifo. Ni Mwokozi ndiye aliyelipa adhabu ya thamani ya dhambi na uvunjaji sheria wetu na kuzifuta kwa masharti ya toba yetu. Ni Mwokozi ndiye anayetukomboa kutokana na kifo cha kimwili na cha kiroho.

Maneno matakatifu kama vile Upatanisho na Ufufuko yanaelezea kile Mwokozi alichokifanya, kulingana na mpango ule wa Baba, ili kwamba tuweze kuishi kwa matumaini katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika ulimwengu ujao.

Chapisha