2022
Yesu Kristo Anatupatia Matumaini
Septemba 2022


“Yesu Kristo Anatupatia Matumaini,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Yesu Kristo Anatupatia Matumaini

Kadiri tunavyowatumikia wengine, Yesu Kristo anatupatia sisi matumaini ya kwamba mambo yatakuwa mazuri katika maisha yetu sisi wenyewe.

Picha
wavulana wakisukuma toroli

Wavulana kutoka Cusco, Peru, wakifanyakazi pamoja ili kutoa huduma.

Maisha haya yamejaa changamoto nyingi. Pengine wewe umeishazipitia baadhi tayari. Kuna visababishi vingi vya msongo wa mawazo na mashaka, hofu na wasiwasi. Wakati tunapopitia mambo haya, mwelekeo ni sisi kugeukia ndani—kujijali sisi wenyewe na shida zetu wenyewe juu ya mengine yote. Tunafikiri kwamba kama tutatumia muda wetu na nguvu zetu tukijaribu “kurekebisha” mambo, tutaweza kuyatatua matatizo yetu wenyewe.

Lakini Yesu Kristo anatuonyesha njia iliyo bora zaidi. Yeye alifundisha: “Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na ye yote atakayeiangamiza ataiponya” (Luka 17:33). Njia ya haraka ya kupata matumaini katika majaribu yako ni kuugeuza moyo wako kwa Bwana na kufuata mfano Wake na kuwahudumia wengine.

Picha
Yesu Kristo anamponya mwanaume huko Bethesaida

Uponyaji huko Bethsaida, na Gary Smith

Maisha ya Mwokozi yalikuwa mfano mkamilifu wa upendo na ukarimu kwa wanadamu. Daima alijisahau Yeye Mwenyewe kwa niaba ya wengine. Matendo Yake yasiyo na uchoyo yalidhihirika katika yote aliyofanya kila siku ya maisha Yake na hayakuishia kwenye majira maalumu.

Tunapoigeuza mioyo yetu kuelekea nje kama Mwokozi alivyofanya, ninaweza kukuhakikishieni kwamba tutaona fursa nyingi za kujitolea kimya kimya na kwa ukarimu kwa watu wanaotuhitaji sisi.

Hii itatusaidia sisi kuja kumjua Mwokozi vyema zaidi na kujionea wenyewe amani duniani kadiri tunavyokuza hisani zaidi kuwaelekea wengine. Unapo “poteza maisha yako” katika kuwasaidia wengine, ukifuata mfano wa Mwokozi, Yeye atakusaidia wewe.

Picha
wavulana wakibeba matofali ya udongo

Malaika wa Kila Siku

Mara kwa mara Mwokozi atawaelekeza wengine kuja katika maisha yetu ili wasaidie kuleta amani na faraja tunayohitaji katika nyakati za jaribu. Watu hawa wenye heri wanaonekana kwetu kama malaika waliotumwa kutoka mbinguni, kwani hakika wametumwa.

Mimi na familia yangu tumeguswa katika matukio mengi tofauti kwa hisia za faraja na amani ambazo jeshi la malaika wa siku za mwisho linaweza kuleta. Ningependa kuangazia juu ya moja ya matukio hayo. Mwaka 2003, tulihama kutoka nchi ya nyumbani kwetu ya Brazili na kuhamia Utah, Marekani.

Majira yale ya baridi, tulipata moja ya dhoruba kubwa ya theluji ambayo haijapata kutokea Utah kwa miaka mingi. Hatukuwahi kuona kitu chochote kama hicho katika maisha yetu, kwani tumekulia kwenye minazi na fuko zenye mchanga. Nyumba yetu ilikuwa kwenye kona kilimani ambayo ilikuwa na njia ndefu pembeni ya waendao kwa miguu.

Theluji ilipoanza, mke wangu kwa ujasiri akaanza kuipuliza theluji njia ya kuingia nyumbani na gari na za waenda kwa miguu. Nilishindwa kumsaidia kwa sababu nilikuwa nimetereza kwenye barafu na nikavunja kiwiko cha mkono siku chache tu kabla yake. Ajali hiyo iliishia katika upasuaji na kufungiwa bandeji ngumu kubwa mkononi.

Alipoanza kupuliza theluji kwenye eneo hilo kwa mara ya kwanza katika maisha yake, mke wangu kipenzi alikuwa hana wazo kwamba ingembidi kubadilisha mwelekeo wa chuti baada ya kusafisha upande mmoja wa barabara. Hivyo basi, alipokuwa akienda upande mwingine ili kusafisha, kumbe huko ndiko upande ile chuti inakoelekeza theluji hiyo. Nyuma na mbele alienda, pasipo mafanikio. Ni vurugu gani hii!

Kwa sababu ya kuwa kwenye baridi kwa muda mrefu, alipata maambukizi ya sikio mara mbili na alikaribia kuwa kiziwi kabisa kwa miezi miwili. Wakati huo huo, mvulana wangu wa umri wa miaka 16 alikuwa amejiumiza mgongo wake wakati akiondoa theluji na alilazimika kulala kitandani ili apate kupona. Tukawa hivyo, mmoja kitandani, mmoja kiziwi, mmoja kafungwa bandeji kubwa ngumu, na sote tunapigwa na baridi.

Nina hakika tulionekana vituko kwa majirani zetu. Katika mojawapo ya hizo asubuhi za baridi kali karibia saa 11:00 alfajiri, niliamshwa na sauti ya kipuliza theluji nje ya dirisha langu. Nilichungulia dirishani na nikamwona jirani yangu ng’ambo ya barabara ya mtaa, Kaka Blaine Williams. Akiwa na umri takribani miaka 70, alikuwa ameacha nyumba yake yenye joto na faraja na kimya kimya alikuwa amekuja na kuiondoa ile theluji kwenye barabara na njia za pembeni, akijua kwamba hatukuweza kufanya hivyo sisi wenyewe.

Picha
kipulizatheluji

Picha kutoka Getty Images

Rafiki mwingine, Kaka Daniel Almeida, alifika nyumbani kwetu ili anipe lifti kwenda Jijini Salt Lake kazini, kwani nisingeweza kuendesha gari kutokana na bandeji ile kubwa niliyofungwa. Wao walikuwa hapo kila asubuhi, wakionyesha upendo wao kwa matendo haya rahisi ya ukarimu, hadi familia yangu ilipokuwa imepona na kuwa na uwezo wa kufanya mambo sisi wenyewe.

Wakati wa majira hayo ya baridi ya 2003 akina kaka hawa wa kimalaika walitumwa kwetu. Hawa akina kaka wawili walifuata mfano wa Mwokozi na wakafikiria mahitaji yetu kabla ya kufikiria yao wenyewe.

Mwokozi Anatupatia Amani

Kuwahudumia wengine kunatupatia mtazamo wa juu zaidi na mtakatifu zaidi. Kadiri tunavyowatumikia wengine, Yesu Kristo anatupatia sisi matumaini ya kwamba mambo yatakuwa mazuri katika maisha yetu sisi wenyewe.

Tunapogeuza mioyo yetu kuelekea nje kama Mwokozi alivyofanya kutatubariki na fursa zisizo na kikomo za kujitolea kimya kimya na kwa ukarimu kwa watu wanaotuhitaji sisi. Kuishi kama Mwokozi alivyoishi pia kunatusaidia kukuza hisani kama ya Kristo kwa watu wengine. Hii inatusaidia sisi kupata kipimo kikubwa zaidi cha upendo, amani, nuru, na kupokea nguvu mpya.

Picha
akina dada

Mwokozi anatualika sisi tumtafute Yeye katika kila wazo na tumfuate Yeye. Hii inatupa sisi ahadi kwamba tunaweza kutembea katika nuru Yake na kwamba mwongozo Wake unazuia nguvu ya giza katika maisha yetu. Kadiri “unavyoyapoteza” maisha yako ndani Yake, Yeye atakusaidia kujitambua.

Picha
wavulana shuleni

Picha kutoka Getty Images

Mgeukie Kristo, Daima

Ninatoa ushahidi wangu wa dhati kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu na kwamba Yu hai. Ninashuhudia kwenu kwamba kupitia Kwake na Upatanisho Wake usio na mwisho, Mwokozi alitupatia njia ya kushinda mauti, yote ya kimwili na kiroho.

Kwa nyongeza, Yeye pia anatupatia faraja na uhakikisho katika nyakati ngumu. Ninakuhakikishieni kwamba tunapomtumaini Yesu Kristo na katika dhabihu Yake ya kulipia dhambi, tukivumilia katika imani yetu hadi mwisho, tutafurahia katika ahadi za mpendwa wetu Baba wa Mbinguni, anayefanya kila kitu kilicho ndani ya uwezo Wake ili kutusaidia sisi kurudi kwenye uwepo Wake siku moja.

Chapisha