2022
Yesu Kristo Anaweza …
Septemba 2022


“Yesu Kristo Anaweza …,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Njoo, Unifuate

Mithali; Mhubiri; Isaya

Yesu Kristo Anaweza …

Kweli zilizoandikwa maelfu kadhaa ya miaka iliyopita zinatufundisha juu ya kitu ambacho Bwana anaweza kukufanyia wewe leo.

Yesu Kristo na Petro wakitembea juu ya maji

Mkamilishaji wa Imani, na J. Alan Barrett

Hakuna tarehe ya mwisho wa matumizi juu ya ukweli kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu ni maarifa “ya vile vitu vilivyo, na vile vitu vitakavyokuwa” (Yakobo 4:13).

Kweli zilizoandikwa maelfu kadhaa ya miaka iliyopita katika agano la Kale bado ni kweli sasa. Na baadhi yake zinakusaidia wewe kuona kitu ambacho Bwana anaweza kukufanyia wewe leo. Hapa kuna baadhi ya kweli hizo kutoka katika vitabu vya Mithali, Mhubiri, na Isaya (ambavyo mtakuwa mkijifunza mwezi huu). Zinakuonyesha wewe kwamba Yesu Kristo anaweza.

Anaongoza Njia Zako

Nyakati zingine, sote tunajisikia kuchanganyikiwa, kupotea, au kuhitaji mwongozo. Kama utampa Bwana matumaini kamili, unyenyekevu, na shukrani, “Naye atayanyosha mapito yako” (ona Mithali 3:5–6).

Kama unashika amri Zake, Yeye “atakuongoza katika njia ikupasayo kuifuata” na kufanya “amani yako … kama mto” (Isaya 48:17–18).

Yesu Kristo na mvulana

Kukutana na Mwokozi, na Jen Tolman

Inakupatia Mtazamo

Mitazamo na mitindo ya maisha katika ulimwengu inaweza kuonekana ya kuvutia na kupendeza. Lakini mafundisho ya Yesu Kristo yanaweza kukusaidia wewe kuona jinsi njia za ulimwengu zilivyo tupu na za kupita tu.

Kila kitu “kifanywacho chini ya jua … ni ubatili na kujilisha upepo” (Mhubiri 1:14). Kwa maneno mengine, njia za ulimwengu huleta mkanganyiko. Ni kama kufukuza upepo na kujaribu kuukamata. Furaha huja wakati tunapotoa heshima na unyenyekevu kwa Mungu na kushika amri Zake (ona Mhubiri 12:13).

Watu wengi katika ulimwengu “huita uovu wema, na wema uovu; … watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; … watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu” (Isaya 5:20). Lakini Yesu Kristo anatuonyesha ukweli. Kwa kufuata njia Yake na neno, ninyi “mtatoka kwa furaha, na mtaongozwa kwa amani” (ona Isaya 55:8–12).

(Ona pia Isaya 40:6–8; 51:7–8.)

Kusamehe Dhambi Zako

Sisi sote tunafanya makosa. Sisi sote tumetenda dhambi. Lakini kama tutatubu na kuendelea kujitahidi kushika amri za Mungu, Yesu Kristo anaweza kutufanya tuwe safi na wazima tena. “Naye ataturehemu [sisi]; … kwani atatusamehe kabisa” (Isaya 55:7). Yeye amesema:

“Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”Isaya 1:18

“Mimi, hata Mimi, ndiye niyafutaye makosa yako … wala sitazikumbuka dhambi zako” (Isaya 43:25).

Yesu Kristo akimkumbatia mtu

Picha na Mark Mabry

Anakuimarisha Wewe

Sisi sote tunajisikia wadhaifu au tumechoka wakati mwingine. Yesu Kristo anaweza kukupatia nguvu. “Maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele” (Isaya 26:4). Endapo utakuwa mnyenyekevu na mwenye kutumaini katika Yeye, Anaweza kukusaidia kushinda majaribu, kufanya maamuzi magumu, au kukuwezesha kusonga mbele licha ya magumu. Yeye amesema:

“Usiogope; kwa maana mimi ni pamoja nawe, usifadhaike; kwa maana mimi ni Mungu wako: nitakutia nguvu; naam, nitakusaidia” (Isaya 41:10).

Kamwe Hatakusahau

Mwokozi Yesu Kristo alijitoa dhabihu Yeye mwenyewe kwa ajili yako kwa sababu Anampenda Baba yetu wa Mbinguni—na kwa sababu anakupenda wewe. Dhabihu Yake imefanya uwezekano wa wewe kufufuka na kupata nafasi ya kuwa kama Baba wa Mbinguni. Kamwe hatakuacha wala hatakusahau. Yeye amesema:

“Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye … ? naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

“Tazama nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu” (Isaya 49:15–16).

Kwa vile Yeye amefanya mengi sana kwa ajili yetu na kamwe hatatusahau, sisi, pia, tunapaswa kujitahidi “daima kumkumbuka Yeye” (Mafundisho na Maagano 20:77, 79).