2022
Kitu Ambacho Ark Anapenda Kujifunza
Septemba 2022


“Kitu Ambacho Ark Anapenda Kujifunza,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Kitu Ambacho Ark Anapenda Kujifunza

Nchi mpya, utamaduni mpya, marafiki wapya … hakuna matata!

Picha
mvulana

Picha na Clayton Chan

Ark anapenda chakula chenye pilipili. Huu ni ugunduzi mpya kwake yeye. Nyumbani Ufilipino, alikokulia, ladha ya vitu haikuwa kali sana.

Lakini baadae baba yake akapata kazi huko Malaysia.

Kwa wakati huo, Ark alikuwa amekutana na marfiki Kanisani ambao wamekuja kutoka katika asili zote, ikijumuisha wachache kutoka India.

“Wanakula vyakula vyenye pilipili nyingi!” Ark C., mwenye umri wa miaka 14, anasema kuhusu marafiki zake wapya. “Chakula hiki kina pilipili nyingi zaidi kuliko nilichozoea kula kule nyumbani.”

Kitu cha kushangaza, ni kwamba—Ark kamwe hakujua ni kitu gani alikuwa anakikosa. Sasa alifurahia kuvinjari ulimwengu wenye mapishi mapya kabisa.

Ndiyo, hiyo sio njia pekee ya marafiki wa Ark walivyoyabadilisha maisha yake na kuwa bora zaidi. “Nilifurahia kuhamia Malaysia, lakini nikihuzunika kwa wakati huo huo. Ilikuwa marafiki wote wapya, na ilikuwa vigumu kuongea na marafiki wapya.

Lakini vijana katika tawi lake jipya walimsaidia kufanya mabadiliko hayo. Kama zawadi, sasa anajua mambo mengi kuhusu maeneo mengi tofauti. “Nimejifunza kuhusu tamaduni tofauti,” anasema. “Chakula ni tofauti, na mavazi pia. Mavazi yao ni ya rangi nyingi, na inashangaza jinsi wanavyoyatengeneza!”

Picha
vijana wakila chakula

Kulikuwa na kikundi kimoja cha marafiki, hata hivyo, ambacho kilimfanya atende zaidi kuliko kikundi kingine cho chote wakati wa na baada ya kuhamia: familia yake

Michezo pamoja na Marafiki

Ark anapenda kutumia muda wake pamoja na familia yake, hasa wanapocheza mchezo wa karata. Mchezo Uno huu ndio mchezo wake mahususi. Sababu ni nini? “Daima ninashinda,” anasema na kucheka.

Pia anapenda kucheza Monopoli pamoja na wazazi wake na mdogo wake, Leaf. (Dada yake mdogo siyo mkubwa vya kutosha kuweza kujiunga nao mchezoni.) Kuna mengi yanayoendelea ndani ya michezo, hata hivyo, kuliko kuchekecha kete na kutumia fedha za bandia, “Wazazi wangu wananifundisha mikakati ya kibiashara na kanuni za fedha katika michezo. Ni ushauri wenye msaada kwa ajili ya wakati ujao”

Baba yake ni mtengenezaji wa software za komputa, na mama yake alikuwa akiendesha biashara yake mwenyewe huko Ufilipino. Wanao ujuzi mwingi wa kuwafundisha wengine. Kwa sehemu yake, Ark ana hamu ya kujifunza kila awezalo kutoka kwao. Ana mpango mkubwa kwa ajili ya taaluma yake.

Picha
familia

Masomo yake ya shule ayapendayo ni biotech na uhandisi. Ark anataka kuwa fundi wa biotech. Pamoja na malengo yake kuyaweka juu, anachukua kila nafasi ya kujifunza kitu kipya.

Kujifunza kutoka kwa wazazi wake , ingawa, hakikuwa daima chanzo cha elimu anachokipendelea. Kama kupenda kwake chakula chenye pilipili nyingi, ugunduzi huu wa nyenzo ya thamani ulikuja baadae kidogo katika maisha yake.

Kutoka Kiburi hadi Mwanafunzi

“Nilizoea kuwa mwenye kiburi sana,” Ark anakiri. “Kwa hakika sikujali kuhusu kujifunza kutoka kwa wazazi wangu.

Angejitahidi kufanya pekee yake au ajifunze kutoka kwa marafiki zake na walimu wa shule pekee. Kisha akasoma kitu kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambacho kilifanya tofauti kubwa katika jinsi anavyovitazama vitu.

Katika Alma mlango wa 36 na 37, Alma anatoa ushauri kwa mwanae Helamani. Alma anamfundisha Helamani kuhusu kila kitu, kutoka kwenye hadithi ya kukumbukwa ya uongofu wa Alma mwenyewe (ambayo inajumuisha siku tatu za kutojitambua baada ya malaika kumwambia yeye kwamba hakuwa akifanya chaguzi sahihi [ona Alma 36:6–10]) hadi kwenye hatari za makundi ya siri.

Katikati ya hili lote, mstari mmoja ukaruka nje ya ukurasa hadi kwa Ark: “Ee, kumbuka, mwana wangu, na ujifunze hekima katika ujana wako; naam, jifunze katika ujana wako kushika amri za Mungu” (Alma 37:35).

Kitu fulani kikashtuka katika akili ya Ark kwa maneno yale. “Wazazi wangu wanaweza kunifundisha mimi hekima pia,” anasema. Kwa wakati mmoja akatambua alikuwa na utajiri wa taarifa mbele yake tu. “Sasa ninajali sana kuhusu hekima yao. Wananipenda na wanaweza kunisaidia kujiandaa kwa maisha yangu ya baadae.”

Na hekima yao inaenda mbali zaidi kuliko mbinu za biashara wanazoshiriki nami wakati wa michezo.

Hekima ya Mama na Baba

Moja ya somo la thamani ambalo wazazi wa Ark wamemfundisha mtoto wao ni kutokuruhusu ushawishi mbaya unaomzunguka kumfanya achanganyikiwe. “Hapa shuleni kwangu, watoto wengi wanataka nijaribu kunywa kahawa, chai, sigara, na kadhalika.”

Hii ni mada ya kawaida ya maongezi ya nyumbani. “Nimekuwa na maongezi mengi na wazazi wangu kuhusu hili. Wanajirudia rudia wao wenyewe mara nyingi,” anatania.

Bado, marudio haya yote yamelipa. Kila wakati anapoombwa kufanya kitu kinyume na imani yake, Ark anachota nguvu kutoka katika kile wazazi wake wamemfundisha.

Somo jingine ambalo amelichukua moyoni ni jinsi ya kuvaa. Hapana, Ark hakuhitaji ushauri juu ya mtindo wa kuvaa kutoka kwa wazazi wake ili aweza kukubalika vyema shuleni. Ukweli, alikuwa akifanya vyema kidogo katika idara hiyo. “Nilizoea kuvaa mavazi yote mazuri,” Ark alisema. “Nilikuwa nikijaribu kuwavutia wasichana.”

Wazazi wake walimsaidia kuona, ingawa, kwamba kulikuwa pia na baadhi ya matokeo yasiyo tarajiwa kwa kuvaa namna hiyo. “Mavazi tunayovaa yanaweza kuwashawishi watu wengine wafikirie kuhusu wewe,” Ark anafafanua. Alipokuwa akifuatilia kwa karibu, Ark aligundua kwamba hakupenda baadhi njia ambazo baadhi ya watu walionekana kufikiria juu yake alipokuwa amevaa nguo kama alivyovaa hapo awali.

Sasa anachagua yenye kulinda heshima, yenye staha—au, kama anavyopenda kuyaita, “mavazi ya”—heshima. Anapenda mwonekano wake mpya na anajisikia vyema zaidi kiroho kuhusu jinsi anavyovaa. (Aidha, mavazi ya Ark, yanapendeza! Ukweli usiopingika.)

Kujifunza Maisha Yote

Ark anapenda mahali anapoishi, anaipenda familia yake, na anapenda kujifunza kutoka kwa wazazi wake.

Pia anapenda kujifunza injili.

Picha
mvulana akisoma

“Ninaamini kwamba Yesu Kristo yu hai,” Ark anasema. “Ninaamini nabii wetu aliye hai ni Rais Russell M. Nelson na kwamba kupitia Joseph Smith, Yesu Kristo amerejesha Kanisa Lake. Ninaamini injili inaweza kutusaidia sisi katika maisha yetu na kuvuka vikwazo vyo vyote, au majaribu tunayopitia.”

Bila kujali yale mambo makubwa Ark anayokwenda kujifunza siku za usoni, tayari amekwisha kujifunza baadhi ya mambo muhimu zaidi ya yote. Karibia na juu ya orodha kuna hii: kutumia muda pamoja na familia kunaongeza msisimko kwenye maisha!

Chapisha