2022
Daraja la Uaminifu
Septemba 2022


“Daraja la Uaminifu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Misingi Imara

Vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho, wanajenga maisha yao juu ya Mwamba wa Yesu Kristo (ona Helamani 5:12).

Daraja la Uaminifu

Picha
msichana akiwa shuleni

Kielelezo na Katie Payne

Shuleni, mwalimu wangu wa kemia alitaka kukuza uaminifu katika darasa lake. Alituambia kwamba tutasahihisha mitihani yetu sisi wenyewe na kutoa ripoti ya alama zetu wenyewe. Nilipokuwa nikikagua majibu yangu, nilijaribiwa niongeze alama moja kwenye alama zangu. Nilihitaji alama hiyo moja tu ya ziada ili kufaulu mtihani huo. Nilikaa hapo kwa muda, nikiwaza nini cha kufanya.

Wakati nimekaa hapo nikifikiria, ghafla nikakumbuka nukuu kutoka kwa Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) ambayo nilikuwa nimeiweka nyuma ya kadi yangu ya utambulisho: “Ni kitu kiharibifu kilichoje kutokuwa mwaminifu kidogo. … Taasisi yaweza kuhimili upotevu wa fedha, lakini mtu huyo haweza kumudu upotevu wa kuji-heshimu” (“I Believe,” Ensign, Aug. 1992, 5). Chini ya nukuu hiyo kulikuwa na kifungu cha maneno: “Kama Mwokozi angesimama pembeni yangu, ningefanya mambo ninayofanya?”

Nilijisikia mwenye amani na furaha nilipojua kile nilichopaswa kufanya. Sikubadilisha alama zangu za kufeli, lakini nilijua kwamba nimefaulu mtihani muhimu zaidi—mtihani wa uaminifu—na niliona fahari kwa uchaguzi niliofanya.

Natalie A., Philippines

Chapisha