2022
Mtanziko wa Kuhama
Septemba 2022


“Mtanziko wa Kuhama,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Misingi Imara

Vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho, wanajenga maisha yao juu ya Mwamba wa Yesu Kristo (ona Helamani 5:12).

Mtanziko wa Kuhama

Familia yangu ilihama hama sana wakati nikikua. Kuzoea maeneo mapya ilikuwa vigumu, lakini nilipokuwa mwaka wa kwanza katika shule ya upili, nilipenda tulipokuwa tukiishi. Kila kitu kilibadilika, ingawa, babu alipofariki na wazazi wangu waliamua kuhamia karibu na bibi yangu. Niliota tukihama tena. Nilifanya kazi kwa bidii ili kuweza kushiriki shuleni na kupata marafiki.

Nikaja kuwa mwenye kukasirika na nikibishana na wazazi wangu kuhusu kuhama. Wazazi wangu walinihimiza kuomba kuhusu jambo hili. Nilijaribu lakini sikupokea majibu yo yote. Licha ya kukatishwa kwangu tamaa, niliamua kuomba mara ya mwisho. Kabla ya kuweza kuanza, nilisikia sauti dhahiri akilini mwangu ikisema, “Rachel, haupati jibu kwa sababu wewe hutaki jibu.” Nilishangaa. Baada ya muda, nilianza kusali tofauti. Niliumimina moyo wangu kwa Baba wa Mbinguni na nikamwuliza Yeye alitaka mimi nifanye nini.

Hisia niliyopokea ilikuwa kwamba familia yangu ilihitaji kuhama. Baada ya kujinyenyekeza mwenyewe na kukubali kile Baba wa Mbinguni alikitaka, nilijisikia mwenye amani. Haikuwa daima rahisi, lakini nilijua kuwa tuko mahali ambako Bwana alihitaji tuwe. Tukio hili lilinisaidia mimi kusogea zaidi kwa Mwokozi wangu na kuhamia karibu zaidi ili kuwa mtu yule Yeye anayehitaji mimi niwe.

Rachel H., Washington, Marekani

Chapisha