2022
Je, kuna ukomo wa mara ngapi ninaweza kutubu?
Septemba 2022


“Je, kuna ukomo wa ni mara ngapi ninaweza kutubu?” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Kwenye Hoja

Je, kuna ukomo wa ni mara ngapi ninaweza kutubu?

wavulana wakichukua sakramenti

Unapotamani kwa dhati kutubu, inaweza kuwa ya kukatisha tamaa unapoteleza tena. Lakini kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo usio na mwisho, huruma na neema ya Mungu visivyo na ukomo, na wewe bado unaweza kutubu na kuwa mwenye kustahili. Kumbuka kwamba “toba siyo tukio; bali ni mchakato” na kwamba “tunapochagua kutubu, … tunachagua … kupokea shangwe.”1

Toba daima inapatikana, hata kama umefanya kosa hilo hilo tena. Bwana amesema, “Na kila mara watu wangu watatubu nitawasamehe makosa yao dhidi yangu” (Mosia 26:30). Uwe mmoja wa “watu Wake,” na rejea kwa Bwana wakati wowote unapokuwa umepotea njia. Pia, ongea na wazazi wako na askofu wako. Msaada wao unaweza kukuimarisha.

Kama unahangaika kuishinda dhambi, usikate tamaa. Shetani yawezekana anataka wewe uamini kwamba wewe ndio chanzo cha kupotea au ulipata nafasi zote unazotakiwa kupata. Lakini si kweli. Endelea kujaribu. Bwana daima anakaribisha toba itokayo moyoni.