2022
Kushiriki sakramenti nyumbani lilikuwa jambo kubwa mno. Kwa nini Bwana anatutaka turudi kanisani?
Septemba 2022


“Kushiriki sakramenti nyumbani kulikuwa jambo kubwa mno. Kwa nini Bwana anatutaka turudi tena kanisani?,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2022.

Maswali na Majibu

“Kushiriki sakramenti nyumbani lilikuwa jambo kubwa mno. Kwa nini Bwana anatutaka turudi kanisani?

Kuwa Walioungana

“Bwana anatutaka turudi kanisani kwa sababu anatutaka tuwe karibu zaidi na Yeye. Pia anatutaka tuwe watu walioungana kama akina kaka na akina dada. Kwa kwenda kanisani, tunakuwa watu walioungana, tunasaidiana, na kumwonyesha Yeye shukrani kwa yale yote Yeye aliyoyafanya kwa ajili yetu sisi. Pia tunaimarisha imani yetu na kujifunza mafundisho mapya.”

Melanie M., 13, Mexico

Nguvu kupitia idadi

mvulana

“Sakramenti nyumbani ilikuwa vizuri kwa sababu ilimleta Roho ndani ya nyumba zetu na ilitusaidia sisi kutambua tunapaswa kulileta kanisa ndani ya nyumba zetu badala ya kufokasi juu yake mara moja tu kwa wiki. Hata hivyo, nyakati zingine kanisa kuwa nyumbani linaweza kukufanya ujisikie upweke. Mtu-kufika kanisani ni muhimu kwa sababu inatengeneza nguvu kupitia idadi.”

Nathan G., 15, Arizona, Marekani

Inajenga Uhusiano

msichana

“Kanisani kuna mazingira ya upendo. Hapo, unaweza kujenga uhusiano na kubariki maisha ya wengine papo hapo nawe ukiwa umebarikiwa. Kanisa pia ni muhimu kwa ajili ya kujenga maarifa yako juu ya injili. Bwana anatutaka tuhubiri injili kwa wale watu wanaotuzunguka na tuijenge Sayuni.

Amelia W., 16, Utah, Marekani

Uwe Hapo kwa ajili ya Wengine

msichana

“Wakati janga la ulimwengu wote lilipoanza, nilihofia tusingeweza kupokea sakramenti, lakini punde askofu akaturuhusu kuipokea nyumbani! Baadhi ya watu wanashangaa kwa nini tunapaswa kurudi tena kanisani, lakini mimi nafikiri lazima turudi ili kuwaangazia wengine—kuongea nao au kumsaidia mtu fulani. Ni lazima twende kanisani kutoa upendo wetu na kushirikiana na wengine uzoefu wetu.

Tamara M., 17, Mexico

Kufanya Upya Maagano

mvulana

“Mungu anatutaka turudi kanisani kwa sababu sio kila mtu ameweza kupokea sakramenti katika nyumba zao. Babu yangu aliniambia kwamba, kama mwanaume mwenye ukuhani, ninapaswa kuhakikisha kwamba kila mtu anapata fursa hii. Ni muhimu kwetu sisi kwenda kanisani ili tuweze kufanya upya maagano yetu.”

Esteban M., 16, Argentina