“Jaribu la Tabia,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Sept. 2022, 18-19.
Misingi Imara
Vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho, wanajenga maisha yao juu ya Mwamba wa Yesu Kristo (ona Helamani 5:12).
Jaribu la Tabia
Hii sio kile nilichojiandikisha kufanya. Nilikuwa radhi vya kutosha kusaidia kutibu ua wa mama ya bibi yangu kwa kupaka mafuta ya kitani ili kusaidia kuukinga. Lakini siku zilivyokuwa zikiyoyoma, jasho likitiririka usoni mwangu na utayari wangu ukageuka kuwa uchovu katika joto.
Mama yangu akapendekeza tupumzike na kunywa kinywaji kabla ya kurudi kazini, lakini mimi nilibibidua midomo, nikidhamiria kuwa mwenye huzuni.
“Dallin, hakuna thawabu halisi kwa kuwa mwenye mtazamo mzuri wakati kila kitu katika maisha kinaenda vizuri,” alisema. “Jaribu halisi juu ya tabia na thawabu ya kweli huja wakati unapoweza kuwa na mtazamo mzuri hata kama kila kitu kinaonekana cha kuhuzunisha.”
Wiki moja baadaye, babu yangu aliuliza kama ninaweza kupaka rangi ua wake kwa mafuta ya kitani. Ua wake ulikuwa mrefu, na tunapaswa kuupaka pande zote mbili.
Wakati huu, nilidhamiria kufanyia kazi mtazamo wangu hata kama kazi ingekuwa ngumu. Tulianza mapema, lakini kwa hakikisho la kutosha, punde tukawa tunaokwa juani. Kazi ilionekana kutokuwa na mwisho tulipokuwa tunabeba zile ndoo nzito za mafuta yenye kunata, na kunuka. Vichaka vyenye miiba pembeni mwa ua vilichoma miguu yetu. Nilipokumbumba kile mama yangu alichosema, ingawa, sikuwa nimelalamika. Lakini sikuacha ile kazi. Nilifanya kazi kwa uangalifu na kujaribu kushikilia mtazamo mzuri.
Tulipomaliza, niliuangalia ukuta ule wa ua uliopakwa rangi na nikaona fahari juu ya kile tulichokifanya. Nilikuwa nimechoka na mwenye kunata, nilijua pia kuwa nimefaulu mtihani muhimu wa tabia. Nilijifunza kwamba ningeweza kuwa na mtazamo mzuri hata kama kila kitu kinaonekana kuwa cha kuhuzunisha.
Dallin H., Oklahoma, Marekani