Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Chagua Nuru!
Januari 2024


“Chagua Nuru,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2024.

Njoo, Unifuate

Ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni; Dibaji ya Kitabu cha Mormoni

Chagua Nuru!

Kitabu cha Mormoni huleta nuru na nguvu katika maisha yako ili kukuongoza katika changamoto na siku za kupendeza zijazo.

Picha
msichana kwenye maandiko

Vielelezo na Gabriele Cracolici

Kama mvulana nilipenda hadithi ya kaka wa Yaredi kwenye Kitabu cha Mormoni. Niliweza kuona uzoefu wake kama sinema katika akili yangu. Ilionekana kama inatokea wakati nikisoma.

Kaka wa Yaredi aliamriwa na Bwana kujenga mashua ili yeye na familia yake waweze kuvuka bahari kuelekea “nchi ya ahadi” (Ether 2:9). Ila mashua zilikuwa na giza. Bila kutaka kusafiri katika giza, kaka wa Yaredi aliomba usaidizi wa Bwana. Bwana aliuliza, “Ungetaka nifanye nini?” (Etheri 2:23).

Kwa imani kubwa, kaka wa Yaredi alibeba mawe16 mpaka kwenye kilele cha mlima na kusali. Alimuomba Bwana kuyagusa mawe “ili yaangaze kwenye giza” (Etheri 3:4). Bwana alinyoosha mkono Wake na kugusa kila jiwe kwa kidole Chake, akiyapa mwanga. Maisha yangu yote, nimevuta taswira Bwana alivyoyagusa mawe yale.

Kama kaka wa Yaredi alivyopewa mwanga, Bwana Yesu Kristo ataleta mwanga kwako. Yeye ni “nuru na uzima wa ulimwengu” (3 Nephi 11:11). Ninakualikeni kuchagua nuru! Kujifunza Kitabu cha Mormoni kutaimarisha imani yako katika Yesu Kristo na kutakusaidia kubaki umeunganishwa katika Mwanga Wake.

Mwongozo na Nuru

Nimesoma Kitabu cha Mormoni na kuhisi ushuhuda mara nyingi kuwa ni cha kweli. Sijawahi kukitilia shaka. Ninapokuwa simhisi Roho, ninapokuwa kidogo niko nje ya mwongozo wa kiroho, ninahisi kiza. Lakini ninaposoma Kitabu cha Mormoni, nuru hurudi. Wakati mwingine hunichukua kusoma mstari mmoja kuhisi nuru tena, ila daima nahisi nuru ninapokisoma.

Nuru kulishinda giza ni dhahiri kwangu. Rais Russell M. Nelson amesema, “Unaposoma kwa maombi Kitabu cha Mormoni kila siku, utafanya maamuzi mazuri—kila siku.”1 Hii ndio sababu Kitabu cha Mormoni huongeza imani yako katika Yesu Kristo. Kinaleta nuru na nguvu. Mafundisho yake yatakuongoza wewe katika siku zijazo za changamoto na za kupendeza.

Kuhisi Nuru

Nina baraka ya kutumikia karibu na Rais Nelson. Wakati nabii anapoingia chumbani, mara moja chumba kinakuwa na nuru zaidi. Anabeba Nuru ya Kristo pamoja naye.

Wakati mwingine ni ngumu kuwa na uhakika kwamba unahisi Nuru ya Kristo. Huwezi kuiona kwa macho ya mwili. Inakuja kama hisia za kiroho. Ni fikra za kipi ni sawa na si sawa na kipi ni kweli na si kweli (ona Moroni 7:13–19).

Muda wowote unapochagua kuwa zaidi kama Yesu Kristo, unatembea katika Nuru ya Kristo. Kusoma Kitabu cha Mormoni huimarisha Nuru hiyo.

“Hakika, Ni Kweli!”

Kwa dhati naamini kwamba wakati maandiko yanaposema,“Kumbuka, kumbuka” (Helamani 5:12), yanamaanisha kwamba hatupaswi tu kumkumbuka Yesu Kristo au kukumbuka kwamba tuliwahi kuhisi Nuru Yake. Tunapaswa kuhisi Nuru Yake sasa na kuihisi tena na tena. Hiki ndicho mvulana mdogo, Eric, aligundua mara ya kwanza aliposoma Kitabu cha Mormoni.

Baada ya kuhamia sehemu mpya na kuanza shule ya upili, Eric alitatizika kwenye darasa lake na kuhisi ilikuwa vigumu kuwa sehemu ya darasa. Pia alianza kujiuliza ikiwa alikuwa na ushuhuda.

“Nilianza kwa bidii kusoma Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza katika maisha yangu,” Eric alisema. “Nilisoma na kusali kila siku.”

Wakati Eric aliposali na kumuuliza Baba wa Mbinguni ikiwa Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, alikuwa na uhakika angepata jibu, lakini hakuna kilichotokea.

Baadaye, akiwa anatembea kwenye kichaka nyuma ya nyumba yake, Eric aliuliza tena. Mara hii, alikuwa na msukumo, kama vile Baba yetu wa Mbinguni alimuuliza, “Eric, nini kimetokea katika maisha yako tangu uanze kusoma Kitabu cha Mormoni na kusali kila siku?”

Eric alitafakari jinsi ambavyo alipata marafiki wapya wazuri na alikuwa akifanya vizuri shuleni. Bila kutambua, Kitabu cha Mormoni kilikuwa kimeleta nuru na nguvu katika maisha yake.

Kisha ilitokea.

“Sikuisikia sauti,” Eric alisema, “ila Roho iliujaza moyo wangu wakati maneno haya yakija akilini mwangu: ‘Hakika, ni kweli!’ Hisia nzito za amani, shangwe na uhakika zilinifunika. Nilijua nilikuwa hatimaye nimepata jibu langu.”2

Songa Mbele katika Nuru

Kutoka ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho, Kitabu cha Mormoni kinashuhudia kwamba” Yesu ni Kristo”3 na kinatufundisha sisi “kipi [tunapaswa] kufanya ili kupata amani katika maisha haya na wokovu wa milele katika maisha yajayo.”4

Kadiri unavyojifunza Kitabu cha Mormoni, natumaini kwamba utahisi kiliandikwa kwa ajili yako. Mafundisho katika Kitabu cha Mormoni na mifano halisi ya Nefi, Lehi na Saria, Abinadi, Alma, Amuleki, Abishi, watoto wa Mosia, na wengine wengi zaidi yatakuinia, kukuongoza, na kukupa nguvu kuwa mfuasi mzuri wa Yesu Kristo na kukuongoza kutembea kwa kujiamini katika Nuru Yake.

Ninashuhudia kwamba Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda wa thamani na uhakika kwamba Yesu Kristo anaishi na ni chanzo cha faraja yetu, tumaini, amani, shangwe na nuru. Ninaomba kwa moyo wangu wote kwamba mtaenda kwenye Nuru ipatikanayo katika Kitabu cha Mormoni, mkisogea karibu na Yesu Kristo, na kuhisi Nuru Yake na upendo ambao hamjawahi kuuhisi hapo kabla.

Picha
Msichana akiwa na penseli na daftari kubwa

Chapisha