Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Rubani katika Jeshi la Bwana
Januari 2024


“Rubani katika jeshi la Bwana,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2024.

Rubani katika Jeshi la Bwana

Lamar F. kutoka Mashariki mwa Midlands ya Uingereza ana malengo makubwa yanayomfanya asonge mbele zaidi, hata pale mambo yanapokuwa magumu.

ndege

Picha zimetolewa na Satomi Folkett

“Nimetamani kurusha ndege kwa muda mrefu kama ninavyoweza kukumbuka,” Lamar F. mwenye miaka 17 anasema. Wakati rafiki yake wa mashindano ya mbio za kiti mwendo alipomwambia kuhusu shirika la msaada la Uingereza ambalo husaidia watu wenye ulemavu kujifunza kurusha ndege, Lamar alikuwa na shauku ya kujaribu.

Ndoto za Angani Juu

Alijiunga na progamu mbili kati ya zile zitolewazo na kituo cha msaada. Mojawapo, Junior Aspiring Pilots Program (JAPP), ilisanifiwa mahususi kwa ajili ya vijana kati ya umri wa miaka 12 na 18. Programu hizi na masomo mengine ya mmoja mmoja yote yalimsogeza hatua moja kwenye lengo lake kuu—Leseni yake Binafisi ya Urubani.

Sehemu ya maono yake inatoka kwenye familia yake. Baba mlezi wa Lamar alikuwa mtu wa kwanza kumuunganisha kwenye ndege, akimpeleka kwenye maonyesho ya ndenge kila mwaka. Baadaye, baada ya kuasiliwa na familia nyingine katika umri wa miaka minne, mapenzi ya Lamar kwenye mambo ya anga yaliendelea kuongezeka kadiri alivyomwona baba yake wa kuasili akisomea leseni yake ya urubani. “Ni mhamasishaji wangu kwa ajili ya kusubiri kuwa rubani, “Lamar alisema. Kwa sasa baba yake na Lamar anaweza kuendesha naye kwenye ndege za rafadha-moja, yenye viti vitano Lamar anajifunza kurusha ndege.

familia

Wazazi wa Lamar (wakiwa kwenye picha hii) ni kati ya waungaji wake mkono wakubwa.

mvulana akisimama karibu na ndege

Katika mruko wa kwanza wa Lamar kwenye ndege halisi, alijihisi mwenye wasiwasi juu ya kukumbuka kila kitu. “Nilitoa sala ya haraka, ya kimya kimya kabla ya kusonga juu, na nilikuwa sawa,” alisema. Sasa anapojitahidi kukumbuka kitu chochote angani, zile sala ndogo, za kimya kimya humsaidia kufanya kile anachohitaji kufanya. Hata pale baba yake anapokuwa hayupo kiti cha nyuma, Lamar daima anajua kuwa yupo na Baba yake wa Mbinguni pamoja naye.

mvulana akiwa ndani ya ndege

Jeshi la Bwana

Kuruka na ndege si kitu pekee kinachofanya roho ya Lamar kufurahia. “Nimekuwa daima mpenzi mkubwa wa jeshi la Uingereza, kila kitu kuanzia msafara wa kifalme hadi mazishi,” anasema.

mvulana akiwa na sanamu za askari
mvulana akipaka rangi kiatu

“Kwa sababu ya ulemavu wangu, siwezi kujiunga na jeshi mwenyewe,” Lamar anasema. Ila mmoja wa viongozi wake wa Wavulana ambaye aliwahi kuwa mwanajeshi amamtia moyo Lamar. “Daima alinikumbusha kuwa sihitaji kuwa kwenye jeshi la dunia kwa sababu tayari nipo katika jeshi la Bwana,” Lamar anasema. “Kuwa katika jeshi la Bwana hunifanya nijihisi kwamba bila kujali nini maisha huleta kwangu, bila kujali ni nini kila mtu hufanya kwangu, nina Yesu Kristo upande wangu.

mvulana na mwanaume

Kaka Bayliss, kiongozi wa Wavulana wa Lamar, alimhamasisha kujiunga na “Jeshi la Bwana.”

Kwenye chuo cha watu wenye mahitaji maalumu anachohudhuria, Lamar anajaribu kuwasaidia watu wa umri wake kujiunga na jeshi la Bwana anaposhiriki injili pamoja nao. “Muda mwingi, hawanijali,” alisema, “lakini wakati mwingine, navutiwa. Kwa sababu ya mahitaji yangu kwa sasa, kutumikia misheni ya muda wote hivi karibuni haitawezekana. Ila naiona kama hivi: sihitaji kibandiko cha jina kuwa mmisionari.”

Wakiwepo vijana wachache katika kata, rafiki zake Lamar wengi si waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hii mara zote si rahisi shuleni, hasa panapokuwepo, kama Lamar anavyoeleza, “mzigo halisi” wa majaribu. “Kuna wanafunzi wengi wanaoongea mambo yasiyo na maadili na kusikiliza miziki isiyo na maadili. Kimsingi, pale kitu kama hiki kinapojitokeza, huwa naondoka na kwenda chumbani ambako huko hakuna hilo.”’

mvulana na bendera

Baki Imara

Wakati majaribu yapokuja au wengine hawataki kusikiliza kuhusu injili, Lamar hutoa andiko analolipenda: “Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana” (Yoshua 24:15).

“Andiko hili limenifanya kubaki imara katika imani ya Yesu Kristo,” anasema. Hii ni muhimu sana kwa Lamar na familia yake. Wakati Lamar akiwa na umri wa miaka 10, baba yake aliacha kwenda kanisani. “Nilikuwa mdogo wakati huo, hivyo kiujumla sikuelewa,” anasema. “Nilijitahidi kumshawishi arudi tena. Ila nimejifunza si kuhusu hicho. Wape muda.”

Lamar bado ana uhusiano na baba yake na humuonyesha upendo kila siku katika kila njia, kama kumsimulia kilichojiri kanisani au kuwa na muda wa kukaa naye. “Daima alinifundisha kwamba pasipo kujali unayoyapitia, unapaswa kubaki imara.” Kwa kijana yeyote mwenye wanafamilia ambao si washiriki kikamilifu Kanisani, anaongezea, “Baki imara. Shikilia imani yako. Usikate tamaa, bila kujali chochote.”

Yesu Kristo

Kumtafuta Kristo Wakati Mambo Yanapokuwa Magumu

Lamar pia amepata nguvu katika Kristo katika njia zake binafsi. “Wati mwingine huteseka na hofu,” Lamar anasema. “Nafikiri mtu wa mwisho wa kunipa mimi ujasiri wa kusonga mbele ni Yesu Kristo Mwenyewe. Alipitia mengi, bado Aliendelea na misheni yake.”

Wakati Lamar anakuwa na siku mbaya, mara zote humfikiria Mwokozi akimtia nguvu, akisema, “Unaweza kufanya hiki. Unaweza kupita katika kila jambo.”

Pia hupata nguvu kutoka kwa baba na mama yake, rafiki zake na watu wengine walio karibu naye. “Kulikuwepo na nyakati wakati nillipoongozwa kwenye njia isiyo sahihi,” Lamar anasema. Ila nashukuru kwa mfumo mzuri wa uungaji mkono, aliweza kurekebisha njia yake na kuimarisha ushuhuda wake juu ya Kristo.

“Bado naendelea kukuza ushuhuda wangu,” anasema, “lakini ni furaha kuwa sehemu ya jeshi la Bwana na katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ni kitu ambacho ninakipenda.”

Safari yake inaweza kuwa na milima na mabonde, ila Lamar anajua kipi humwezesha kuendelea kupaa juu. “Bila kujali majaribu au matatizo unayoyapitia, Baba wa Mbinguni atakuwa upande wako kwa sababu Anakujali na anakupenda.