“Kutafuta Mapya,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2024.
Njoo, Unifuate
Kutafuta Mapya
Hapa kuna somo la kufurahisha unaloweza kufundisha familia yako au darasa wakati wa mafunzo ya Njoo, Unifuate ya mwezi huu.
Unapojaribu kitu kipya, unaweza kujihisi kama Nefi akitafuta bamba za shaba “wala hujui kimbele vitu ambavyo [wewe] ungefanya” (1 Nephi 4:6). Ila kumbuka, hauko peke yako, na hasa kama unafanya kitu ambacho Mungu amaeamuru.
1. Bila ya kujua Kile Kitokeacho
Mpe kila mtu kipande cha karatasi. Ila usiwambie ni cha kazi gani. Badala yake, zungumzia jinsi tunavyopata maono kila mara kutoka kwa Mungu hatua moja kwa wakati (ona 1 Nefi 3–4) au kujenga meli (ona 1 Nefi 17–18).
2. Mstari juu ya Mstari
Sasa inakuja sehemu ya kufurahisha! Soma maelekezo haya kwa sauti moja baada ya mengine kusaidia kundi lako kufumbua fumbo lao kwa ufafanuzi. (Ni vigumu, bila picha! Ikiwa watahitaji msaada wa ziada, acha wachukue hatua kwa wakati.)
3. Ufunuo: Kwa kuongozwa na Roho
Familia yako au darasa wanapaswa sasa kuwa na karatasi ambazo zimetengenezwa kuwa boti! Chukua dakika chache kuzungumzia kuhusu nyakati ambapo wote mlihitaji maelekezo ya Mungu mliyohitaji “mstari juu ya mstari.” Wangeweza hata kuandika au kuchora kitu chochote kwenye boti zao kukumbuka nyakati hizo.
Sasa wakati maisha yanaporusha vitu vipya kwako, usisahau kutafuta ufunuo kutoka kwa Mungu. Kumbuka, daima Ataandaa njia kwa ajili yako kufanya kile Alichokutaka ufanye (ona 1 Nefi 3:7).
Maelekezo
-
Shikilia kipande cha karatasi wakati upande mfupi ukiwa juu. Kikunje nusu, juu hadi chini.
-
Kikunje nusu tena kutoka kushoto kwenda kulia, halafu kunjua mkunjo uliotengeneza.
-
Ukiwa na upande uliokunjwa ukitazama juu, chukua kona za juu mbili na uzikunje kwa chini kwenye mkunjo wa katikati. Inapaswa kuonekana kama pembe tatu pamoja na mstatili kwa chini.
-
Shika kipande kidogo cha karatasi kwa chini ya pembe tatu yako na kunja sehemu ya juu. Binua kwa juu na urudie kubinua kwa upande mwingine.
-
Vuta na ufungue kwa sehemu ya chini na sasa inaonekana kama kofia.
-
Endelea kuvuta hadi sehemu za mwisho mbili zikutane na kuwa bapa kama umbo la almasi.
-
Ukiwa na sehemu iliyo wazi kwa chini, kunja sehemu ya kwanza mpaka juu ya umbo la almasi Binua na rudia kwa upande mwingine. Inatakiwa kuonekana kama pembe tatu.
-
Vuta na fungua sehemu ya chini na ifanye bapa kama ulivyofanya kwenye hatua ya 5 na 6 ya umbo la almasi.
-
Umbo lako la almasi linatakiwa kuwa na mibinuko miwili ya pembe tatu kwa upande wa kushoto na kulia. Vuta sehemu hizo kwa nje na uzifanye bapa ili uwe na trapeza juu chini. Baadaye sukuma pembe kwa nje kuisaidia isimame yenyewe.