Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Sehemu ya Burudani
Januari 2024


“Sehemu ya Burudani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2024.

Sehemu ya Burudani

Picha
Sehemu ya Burudani

Vielelezo na Ben Rowberry

Pakua PDF

Mchezo wa Kitabu cha Mormoni wa Kutafuta na Kukusanya

Anza na swali A. Kisha tumia jibu kutoka swali la awali kujaza katika sehemu ya kwanza iliyo wazi katika swali lifutalo. Mwishoni utakuwa na rejeleo la andiko kwa ajili ya kauli mbiu ya vijana ya 2024.

  1. Anza katika 1 Nefi 1:9–10. Ni “wengine” wangapi Nefi aliwaona wamkifuata “Mmoja” (Mwokozi)? __________

  2. Nenda kwenye Omni 1:[A]________. Nani aliwekwa kuwa mfalme katika nchi ya Zarahemla? _______

  3. Nenda kwenye [B]________ 17:2. Nani aliamini maneno aliyosema Abinadi? ___________

  4. Nenda kwenye [C]________ 53:22. Nani aliwaongoza mashujaa 2000? ______

  5. Nenda kwenye [D]_________ 14:2. Katika miaka mingapi Mwokozi angekuja? __________

  6. Nenda kwenye Mosia 6:[E]_______. Miaka mingapi zaidi Mfalme Benjamini aliishi? ___________

  7. Nenda kwenye 2 Nefi [F]______:25. Ni manaeno ya nani Lehi alimwambia Yusufu kuyafuata? ___________

  8. Nenda kwenye 2 [G]_______ 23. Kichwa cha mlango kinasema kulinganisha Isaya ________.

2024 Dhima ya Maandiko: [F]_____ [G]________ [E]_____:[H]______

Andiko hili linamaanisha nini kwako?

Mti wa Uzima: Mzingile

Kuna njia moja inayoongoza mpaka kwenye mti wa uzima. Unaweza kuitambua ni ipi?

Muda wa Tafisiri

Ni mwaka gani ambao Joseph Smith alimaliza kutafsiri bamba za dhahabu? Kupata jibu, utapaswa kufumbua fumbo kwa “kutafsiri” maumbo katika namba yanayoziwakilisha. Pia fanya zoezi la hesabu mwishoni.

Kumbuka: Kila umbo linawakilisha namba moja maalumu. Kwa wale wanaotafuta changamoto, fumbo hili linaweza kufumbuliwa bila dokezo zozote. Ikiwa utakwama, baadhi ya taarifa zimejumuishwa chini ya ukurasa huu.

  1. [pembe tatu] + [pembe tatu] + [pembe tatu] = [mstatili]

  2. [mstatili] – [trapeza] = [pembe sita]

  3. [pembe sita] ÷ [almasi] = [trapeza]

  4. [almasi] x ½[almasi] = 8

  5. [pembe tatu] x [trapeza] = [mstatili]

Swali la Hesabu:

([mstatili] x [pembe tatu]) + (1/2[almasi]) = [umbo la ajabu]

([umbo la ajabu] x [pembe tatu] x [pembe tatu]) + [almasi] – 100 = _______________.

Vichekesho

Picha
kichekesho

Ubaya wa kuwa kaka mdogo wa Goliathi ni kuvaa vazi lake.

Val Chadwick Bagley

Majibu

Mchezo wa Kitabu cha Mormoni wa Kutafuta na Kukusanya

  1. 12

  2. Mosia

  3. Alma

  4. Helamani

  5. 5

  6. 3

  7. Nefi

  8. 13

Maandiko ya Kauli mbiu: 3 Nefi 5:13

Muda wa Tafsiri

1829

Chapisha