“Njia nyingi za kujifunza,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2024.
Njia Nyingi za Kujifunza
Unataka kuufanya ulimwengu kuwa walau bora zaidi? Yote huanza kwa kujifunza namna ya kufanya hivyo.
Kujifunza kunyoa nywele kunahusiana vipi na kupangilia taa za jukwaani?
“Yote ni sehemu ya mpango wangu,” anasema Lisa, kijana mkubwa katika mwaka wake wa kwanza chuoni.
Lisa alianza shule ya mambo ya upambaji katika umri wa miaka 16. Vile vile alipata programu ambayo ingemwezesha kuhudhuria kwa muda mfupi katika shule ya sekondari ili aweze kuhudhuria shule ya upambaji mchana. Ukweli kwamba sasa yupo chuoni akisomea mafunzo ya sanaa ya jukwaani haimaanishi kwamba shughuli zote za saluni hazikuendelea, pia. Kimsingi, kila kitu kinaendelea kama jinsi alivyotumainia.
“Nilitaka kuwa na ujuzi ambao ungenisaidia kulipa kwa ajili ya chuo, “ Lisa anasema. “Zaidi, iliniwezesha kuwahudumia watu wengine na kutunza fedha ambayo ingekuwa gharama ya kunyoa nywele za wanafamilia maisha yote!”
Kwa nini Tunajifunza
“Baba wa Mbinguni anataka binti zake na wanawe siku zote wawe wanajifunza.”1 Hapa kuna baadhi ya njia chache kati ya nyingi ambazo kujifunza maishani ni baraka kubwa:
-
Unaweza vizuri kusaidia na kufundisha marafiki zako, familia na wengine.
-
Unaweza kuhudumu vizuri Kanisani na katika jamii yako.
-
Utakuwa na ujuzi unaohitajika zaidi kwa ajili ya kujitegemea.
-
Utaweza kuwa na maarifa yako baada ya kifo.
-
Kadiri unavyoishughulisha na kuifanyisha kazi akili yako, itabaki yenye afya.
Jinsi Gani Tunajifunza
Kupitia maandiko tunajifunza kwamba tunapaswa “Kutafuta kujifunza, hata kwa kusoma na kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118; ona pia 130:18). Kwa sasa kuna nafasi nyingi za kujifunza kuliko ilivyowahi kuwa, kama vile:
-
Mfumo rasmi wa shule, ikijumuishwa chuo cha kati, chuo kikuu na shule za biashara.
-
Kutafuta maarifa kutoka kwenye vitabu vizuri” (Mafundisho na Maagano 88:118). Unaweza pia kuongeza, “vyanzo vizuri vya kidigitali.”
-
Kujifunza moja kwa moja kutoka kwa marafiki na wanafamilia.
Wazo la shughuli! Tengeneza shughuli ya “kubadilishana ujuzi” katika tawi lako au kata. Kila mmoja anajitokeza tayari kufundisha kitu wanachojua kufanya.
-
Sala na kujifunza maandiko.
-
Kwa uaminifu ishi kwa ustahili wa ushirika wa kudumu wa Roho Mtakatifu, ambaye “atawafundisha mambo yote” (Yohana 14:26).
-
Majaribio, vitu vya ubunifu na juhudi. Kitu kikubwa kuhusu maarifa ni kwamba mengi hufunzwa kila siku. Unaweza kuongeza kwenye hifadhi ya ulimwengu wa maarifa.
Lini Tunajifunza
Hatimaye, iwe unajifunza kunyoa nywele kama Lisa au unajifunza namna ya kuendeleza nguvu za kiteknolojia ya kizazi kijacho, Rais Nelson anatukumbusha kwamba daima kuna muda mzuri kwa ajili ya hayo:
“Ndiyo, tunapaswa kujifunza kutokana na yaliyopita na ndiyo, tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya siku za baadaye,” alifundisha. Lakini ni sasa tu tunaweza kufanya. Sasa ndio wakati tunapoweza kujifunza. … Sasa ndio wakati tunapoweza kubariki wengine.”2
Ndio, sasa. Nini unataka kujifunza leo?