Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Mfuasi wa Yesu Kristo
Januari 2024


“Mfuasi wa Yesu kristo,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2024.

Mstari juu ya Mstari

Mfuasi wa Yesu Kristo

Angalia ni kwa jinsi gani maelezo ya Mormoni kumhusu yeye mwenyewe yanatumika na kwako pia.

Picha
nabii Mormoni

mfuasi wa Yesu Kristo

Neno mfuasi linamaanisha mtu anayejifunza kutoka kwa mwalimu au bwana (kama mwanafunzi au mwanagenzi).

Wafuasi wa Yesu Kristo hujifunza kutoka Kwake, hufuata mafundisho Yake na kuwa kama Yeye.

Huwaita Kutangaza neno lake

Baadhi ya watu wana wito maalumu kutangaza neno la Kristo, kama vile wamisionari. Ila kupitia maagano yetu, tunaahidi kushika amri Zake, ikiwa ni pamoja na amri ya kuwa mwanga kwa ulimwengu (ona Matayo 5:14–16). Na tunatangaza utayari wetu “kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, na katika vitu vyote na katika mahali popote” (Mosia 18:9).

Kila muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ameitwa kukamilisha kazi ya Bwana na kushiriki injili Yake (ona Mafundisho na Maagano 38:40–40).

maisha ya Milele

Maisha ya milele maana yake ni maisha katika ufalme wa selestia pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Hii ni zawadi kwa watu walio na imani katika Yesu Kristo, wametubu, wameweka na kushika maagano na kuvumilia hadi mwisho.

Bwana amesema, “Hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu, kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39). Wafuasi humsaidia Yeye kukamilisha kazi yake.

Chapisha