Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ninahitaji msaada kupanga shughuli za vijana. Je, kuna mawazo yapi mazuri?
Januari 2024


“Ninahitaji msaada kupanga shughuli za vijana. Je kuna mawazo gani mazuri?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2024.”

Maswali na Majibu

Ninahitaji msaada kupanga shughuli za vijana. Je, kuna mawazo yapi mazuri?”

Fanyeni zamu na Kupanga kwa Pamoja

Picha
msichana

“Tunafanya zamu kila wiki kupanga shughuli. Hii huondoa uzito kwa mtu mmoja, na tunapata mawazo mengi. Kuwa na shughuli ambapo wote mmepanga kwa pamoja pia inasaidia. Tunapenda kucheza michezo, kucheka pamoja na kufanya huduma.”

Adelynne S., 17, Utah, USA

Waleta wengine kwa Mwokozi

Picha
msichana

“Waulize washiriki wa darasa lako au akidi nini wanafurahia kufanya. Chagua shughuli ambayo itawaleta vijana kwa pamoja na kwa Mwokozi, na muweze kufurahi kwa pamoja! Shughuli za huduma zimekuwa daima sehemu ya mapendeleo yangu. Daima huwa napata marafiki wapya!

Katie G., 18, Washington, USA

Jaribu kumhusisha kila mtu

Picha
msichana

“Shughuli ambazo kila mmoja anaweza kushiriki inaweza kuwafanya wengine wahisi kukaribishwa. Kuwauliza kundi lako nini mapenzi yao au vitu vingine wanavyofurahia husaidia sana.”

Lily D., 13, Arizona, USA

Maswali Matatu

Picha
msichana

“Darasa langu mara kwa mara hupanga shughuli zilizolengwa katika maswali matatu: Nini tunahitaji kuboresha? Nani tunahitaji kumuunga mkono? Je ni muda kwa ajili ya shughuli ambayo inachukua muda mfupi na nguvu kidogo kuliko shughuli nyingine? Pamoja na mambo haya akilini, tafakari na shaurianeni kwa pamoja. Mmeipata hii!”

Isabella R., 14, Oregon, Marekani

Muundo wa Kiroho

Picha
msichana

“Utahitaji magazeti ya Kanisa mengi ili uweze kukata taswira za kiroho au jumbe ambazo zinakuhamasisha wewe. Pia weka ulichokikata kwenye fremu katika mpangilio maalumu. Unaweza kuweka sehemu ambapo unaweza kuangalia.”

Florence M., 14, British Columbia, Kanada

Chapisha