“Mfuasi hadi Mfuasi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2024.
Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2024
Mfuasi hadi Mfuasi
Ni kwa Jinsi Gani unaweza kuwa mfuasi wa Yesu Kristo? Ni rahisi zaidi kuliko unavyoweza kufikiria. Tazama mifano hii ambayo vijana wanaishiriki kuhusu ufuasi katika maisha yao.
Kyler C., umri 13
Kutoka Guayas, Ecuador. Anapenda kucheza mpira wa kikapu na violin.
Marafiki zangu wawili kutoka kanisani, Arik na Mike, wamenifundisha umuhimu wa kuwa mfuasi wa Yesu Kristo. Mifano yao imenisaidia kuwa na hamu zaidi ya kutumikia misheni. Sasa ninafurahi kushiriki kuhusu Yesu Kristo kwa wale ninaohitaji.
Marafiki zangu pia ni mifano mizuri ya Kristo kwa jinsi wanavyoongea. Wameshiriki uzoefu mwingi pamoja nami kuhusu kumfuata Yesu Kristo, jambo ambalo limenihamasisha kuwa karibu na Yeye. Kwa mfano, rafiki yangu amenifundisha kwamba tunapokuwa na swali, tunaweza kumuuliza Mungu. Na tunajuaje wakati gani Anajibu? Tutajua ndani ya mioyo yetu. Huyu ni Roho anasema Mungu anaongea nasi na kwamba tunachagua njia sahihi.
Ayotunde Raphael A., umri 15
Kutoka Oyo, Nigeria. Anapenda dansi, michezo na kufundisha na wamisionari.
Rafiki yangu Ewa (kifupisho cha Ewaoluwa) ni mfano wa mfuasi wa Kristo. Aliwahi kuniudhi, na nilikuwa mwenye hasira naye. Kisha aliniomba msamaha. Kupitia mchakato huu, nilijifunza unyenyekevu na msamaha kutoka kwake. Alikuwa mnyenyekevu alipoomba msamaha, na nilimsamehe.
Kwangu, kuwa mfuasi wa Yesu Kristo ni kushika amri za Baba wa Mbinguni, kumpenda Mungu na Mwanawe, Yesu Kristo, na kuwajali wengine zaidi.
Gabriel A., umri 12
Kutoka Oyo, Nigeria. Anapenda kucheza mpira wa miguu (kandanda).
Nilimfahamu mvulana kutoka kanisani ambaye alikuwa mwonevu kabla, lakini siku moja ghafla alibadilika. Niliamua kumuuliza, Kwa nini ulibadilika?” Aliniambia kwamba alisali, kusoma maandiko yake, alikuwa na imani na alitia bidii kubadilisha tabia yake. Ilinisaidia kwa sababu sasa ninapotaka kufanya maamuzi, kimasomo au kiroho, daima huwa nasali kupata usaidizi wa Mungu.
Rafiki yangu anaweza asiwe mkamilifu, ila tabia yake iligusa moyo wangu. Sasa huwa nasoma maandiko kabla ya kufanya jambo lolote maishani mwangu. Mifano ya rafiki yangu imenileta karibu na Kristo sababu kila ninapotenda dhambi, naweza kurudi kwa Bwana katika sala na kutubu. Kwenda kwa Bwana kumenisaidia mimi kuweka kando mizigo yangu.