Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Mpendwa
Julai 2024


Mpendwa

Haya hapa ni mashairi ya wimbo huu kutoka katika albamu ya Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2024.

Picha
Mashairi

1. Nimeona picha;

Nimewaona wanawake kwenye skrini zangu.

Ni nzito akilini mwangu

Kwa nini wanaonekana wenye furaha kuliko mimi.

Na nimekuwa nikikimbia pande zote

Kumfukuza mtu ninayepaswa kuwa.

Inaniweka macho usiku kucha.

Matarajio haya daima yanaonekana

Mazito sana. Ninawezaje?

Kupata ukweli wakati ni vigumu sana kuona?

’Sababu ni kama kujaribu kupata

tone ndani ya bahari yenye kina kirefu sana. Mm.

Lakini kisha ninakusikia Wewe ninapojiona mpweke.

Sauti yako inaweza kuniponya,

Niokoe kutoka utu wangu mwenyewe.

Chukua uzito wangu

Na kuutoweshea mbali.

Na ninakumbuka kuwa ninapendwa.

Mimi ni wa kiungu—

Asili takatifu,

Na nimesanifiwa kikamilifu.

Wakati sihisi kuhitajika,

Unaniita—

Ninakumbuka ninapendwa.

Mimi ni wa kiungu—

Asili takatifu,

Na nimesanifiwa kikamilifu.

Wakati sihisi kuhitajika,

Unaniita mpendwa. Mpendwa.

2. Ninaondoa makelele,

Na katika ukimya naweza kuona

Unanipenda kuliko maisha,

Na upendo wako ndio tumaini lote ninalohitaji.

Ushahidi uko katika nyota

Na katika makovu uliyochukua kwa ajili yangu.

Nyakati fulani ninakusikia niwapo mpweke.

Sauti yako inaweza kuniponya,

Niokoe kutoka utu wangu mwenyewe.

Ninajua mimi ni nani

Haijalishi ninaenda wapi.

Ninakumbuka ninapendwa.

Mimi ni wa kiungu—

Asili takatifu,

Na nimesanifiwa kikamilifu.

Wakati sihisi kuhitajika,

Unaniita—

Ninakumbuka ninapendwa.

Mimi ni wa kiungu—

Asili takatifu,

Na nimesanifiwa kikamilifu.

Wakati sihisi kuhitajika,

Unaniita mpendwa. Mpendwa.

Makovu yangu hayanifanyi mimi kuwa nilivyo.

Lo, yanasimulia hadithi yangu tu.

Mapungufu yanafifia,

Na Wewe unanisaidia kuona uzuri.

Makovu yangu hayanifanyi mimi kuwa nilivyo.

Lo, yanasimulia hadithi yangu tu.

Mapungufu yanaisha,

Yanafifia.

Na ninakumbuka kuwa mimi ni mpendwa.

Mimi ni wa kiungu—

Asili takatifu,

Na nimesanifiwa kikamilifu.

Wakati sihisi kuhitajika,

Unaniita—

Ninakumbuka ninapendwa.

Mimi ni wa kiungu—

Asili takatifu

Na nimesanifiwa kikamilifu.

Wakati sihisi kuhitajika,

Unaniita mpendwa. Mpendwa.

Chapisha