Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Je, itakuwaje kama siwezi kusema najua injili ni ya kweli?
Julai 2024


“Je, itakuwaje kama siwezi kusema najua injili ni ya kweli?,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2024.

Kwenye Hoja

Je, Itakuwaje kama siwezi kusema najua injili ni ya kweli?

Picha
mmea ukimwagiliwa maji

Kama hauhisi kwamba unaweza kusema, “Najua,” ni SAWA. Anza na kile unachokiamini. Na kama huna uhakika kuhusu hilo, anza na kile unachotamani kukiamini. Kisha “ruhusu hamu hii ifanye kazi ndani yako” (Alma 32:27) na kukuongoza kutenda—kusali, kusoma, kutubu, kuhudumu. Unapotumia imani, kuwa msikivu kwa mawazo na hisia zako. Baada ya muda, yawezekana ukasema kwa ujasiri, “ninaamini.”

Imani ni neno la thamani, tendo la thamani zaidi, na [huhitaji] kamwe kuomba msamaha kwa ‘kuamini tu.’”

Thamini kweli za injili unazoziamini. Tenda juu ya kweli hizo. Kuwa mwaminifu kwa kweli hizo. Unapofanya hivyo, utabarikiwa na Roho Mtakatifu. Na unaweza kuhisi uko nyumbani ndani ya Kanisa bila kujali ni aina gani ya ushuhuda ulio nao. Kama Rais Dieter F. Uchtdorf, alipokuwa–Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema, “Sijaona alama yoyote kwenye milango ya nyumba zetu za mikutano ambayo inasema, “ushuhuda wako lazima uwe na urefu huu ili uingie.’”

Chapisha