Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Hakuna mtu shuleni anayeshiriki viwango vyangu. Ninawezaje kuwa na marafiki wema huko?
Julai 2024


“Hakuna mtu shuleni anayeshiriki viwango vyangu. “Ninawezaje kuwa na marafiki wema huko?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jul. 2024.

Maswali na Majibu

“Hakuna mtu shuleni anayeshiriki viwango vyangu. Ninawezaje kuwa na marafiki wema huko?”

Picha
msichana

“Zungumzeni kuhusu mambo mnayoyapenda kwa pamoja. Huna haja ya kupunguza nuru yako. Unahitaji tu kuwa kijana wa kawaida ambaye anajihusha na baadhi ya mambo ya burudani ambayo vijana wengine huyafurahia. Fuata viwango vya Yesu Kristo, na uwajulishe wazi wanafunzi wenzako viwango unavyovifuata.”

Jamie Ann B., umri miaka 18, Negros Occidental, Ufilipino

Picha
msichana

“Tafuta watu mlio katika madarasa, mapendeleo, vipaji au michezo sawa. Kuna watu wema wa imani zingine, pamoja na watu wa kupendeza ambao hawana imani hata kidogo. Hawa wote bado ni watoto wapendwa wa Mungu. Unapoendelea kushika viwango vyako, hata marafiki zako wasipofuata, mfano wako unaweza kuwatia moyo wengine wafanye maamuzi bora zaidi.”

Lucy B., umri miaka 15, Lima, Peru

Picha
mvulana

“Kuwa na subira na uwe tayari kujifunza. Urafiki unahusu ubora, si wingi, na kuwa na marafiki wachache wa kweli kunaweza kukupa thawabu zaidi kuliko kujaribu kupatana na umati ambao haupatani na maadili yako.”

Adedoyin Alma O., umri miaka 17, Osun, Nigeria

Picha
msichana

“Shiriki nao viwango vyako. Ikiwa wanajua viwango vyako ni nini, wataweza kuviheshimu. Unaweza pia kuwaalika marafiki zako wa shule kuja kanisani na/au shughuli za Kanisa ili kuwasaidia waone zaidi kile unachokiamini.”

Margarett P., umri miak 13, Texas, Marekani

Picha
msichana

“Nimejifunza kwamba unaweza kupata marafiki wazuri kupitia ushawishi na kwa kuwa jinsi ulivyo tu. Wakati fulani watu watakuja kwako, na wakati fulani lazima uangalie, lakini kutakuwa na watu ambao watakuwa marafiki wazuri au wanaohitaji rafiki mzuri kama wewe.”

Katie R., umri miaka 18, Nebraska, Marekani

Chapisha