Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Unganika
Julai 2024


“Unganika,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2024.

Unganika

Renata B.

12, La Paz, Bolivia

Picha
msichana

Shuleni nilionewa kinguvu na kuonewa mtandaoni. Niliwaambia wazazi wangu kilichotokea, nao wakanisaidia. Na kila siku nilisali kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya uhusiano bora na marafiki zangu na kwamba ningekuwa hodari kukabiliana na kile nilichokuwa nikipitia. Nilihisi amani, na sasa mambo yanakuwa mazuri. Ninajifunza kusamehe wakorofi na sio kuwa na kinyongo.

Nimekuwa na matukio mengine ambapo Mungu amenisaidia. Mimi husema sala kila wakati ninapocheza dansi ya baleti, kwa sababu mimi ninakuwa mwenye wasiwasi sana. Daima inanifanya niwe mtulivu ili nimfikirie Baba wa Mbinguni. Pia nilifanya mazoezi ya kinanda hadi nilipoweza kukipiga kanisani. Hata kama sikufanya kikamilifu, nilitoa juhudi zangu zote na kuona baraka kutoka kwa Bwana.

Chapisha