“Nguvu ya Mashujaa,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Julai 2024.
Nguvu kutoka kwenye Maandiko
Nguvu ya Mashujaa
Mashujaa wa Kitabu cha Mormoni walihitaji nguvu pia, na Yesu Kristo alikuwa ndiye chanzo chake. Unawezaje kuchota nguvu Zake kama mashujaa hawa walivyofanya?
Nefi: Ufunuo (1–2 Nefi)
Kuondoka nyumbani, kupambana na changamoto za familia na kukabiliana na mambo yasiyojulikana kunaweza kuwa vigumu. Lakini alipoweka imani yake kwa Bwana, Nefi alijifunza kutafuta ufunuo na kumtumaini Bwana amwongoze.
Alma na Wana wa Mosia: Toba (Mosia 27–28; Alma 36)
Inahitajika nguvu ili kutubu na kukiri kuwa ulikosea. Baada ya kundi hili la marafiki kupata wito wenye nguvu wa kutubu, walimgeukia Yesu Kristo na kupata nguvu nyingi. Kwa ujasiri waliacha maisha yao ya zamani na, kwa imani, walimtumikia Bwana na kuwasaidia wengine wafanye vivyo hivyo. Walipata furaha kubwa.
Vijana mashujaa: Kupigana Vita vya Maisha (Alma 53: 56–57)
Maisha yana vita vya kila aina. Wakati vijana hawa walipokabiliwa na vita, walikumbuka kitu walichofundishwa na mama zao kuhusu injili na hivyo wakapigana “wakiwa na nguvu za Mungu” (Alma 56:56).