Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Je, Wewe Utasikiliza?
Septemba 2024


Njoo, Unifuate

Helamani 13–16; 3 Nefi 1

Je, Wewe Utasikiliza?

Mwongozo wa nabii unaweza kutulinda, kutubariki, na kutusaidia—kama tutauacha ufanye hivyo.

mvulana katika umati wa watu akiangalia jukuta  na Samweli Mlamani akiwa juu ya ukuta

Vielelezo na Alyssa Talent

“Angamizo linakuja!”

Huo ni ujumbe wa huzuni kuupokea. Lakini fikiria ukiwa ndiye uliyeitwa kuutoa !

Samweli Mlamani aliitwa na Bwana kuwaonya Wanefi juu ya uovu wao. Akiwa amesimama juu ya ukuta, Samweli alitamka kwamba siku moja “angamizo kamili … kwa kweli litakuja isipokuwa mtubu” (Helamani 13:10).

Samweli pia alitoa unabii kwamba katika miaka mitano ijayo patakuwa na usiku usio na giza na nyota mpya katika anga kuashiria kuzaliwa kwa Mwokozi (ona Helamani 14:2–5).

Je, ni namna gani Wanefi waliitikia ujumbe huo wa Samweli?

Walikataa kumsikiliza. Wao “walimtupia mawe [Samweli] … na … walirusha mishale akiwa amesimama kwenye ukuta” (Helamani 16:2). Tushukuru, watu hawatupi mawe au kurusha mishale kwa manabii leo, lakini wengi bado wanakataa na kudhihaki maneno yake anapofundisha kweli za milele za injili ya Mwokozi.

Wakati nabii anapoongea, je wewe utaitikiaje? Je, wewe utasikiliza?

Hapa kuna mambo matatu ya kutukumbusha juu ya baraka ambazo huja kutokana na kuwa na nabii duniani na kumsikiliza.

Nabii Anatupenda na Anatuombea.

Katika mahubiri mengi ya mkutano mkuu, Rais Russell M. Nelson ametuambia:

“Ninawapenda!” “Daima mmekuwa akilini mwangu na katika sala zangu.”

Ni baraka iliyoje kujua kuwa nabii anatupenda na anatuombea!

Takribani miaka mitano baada ya unabii wa Samweli Mlamani, baadhi ya Wanefi walisema muda umepita wa maneno yake kutimizwa. Waliwadhihaki wale walioamini na hata wakachagua siku ya kuwaua waaminifu kama ishara ya kuzaliwa kwa Mwokozi haikuja (ona 3 Nefi 1:6–9). Katika wakati huu wa kuogofya, nabii Nefi alisali siku nzima “kwa niaba ya watu wake … ambao walikuwa karibu ya kuangamizwa kwa sababu ya imani yao” (3 Nefi 1:11).

Leo, sala za nabii zinatusaidia katika njia nyingi zaidi kuliko tunavyoweza kutambua. Mwongozo wa kiroho anaopokea kupitia sala zinaubariki ulimwengu wote.

Nabii Anatuongoza Sisi kwa Mwokozi

“Inua kichwa chako na uchangamke; Bwana alimwambia Nefi. “Wakati umefika, na kwa usiku wa leo ishara itatolewa, na kesho nitakuja ulimwenguni” (3 Nefi 1:13).

Jua lilipotua, hakukuwa na giza. Ile ishara imekuja! (Ona 3 Nefi 1:15). Asubuhi iliyofuata, kila mtu alijua kwamba ilikuwa ndiyo ile siku Mwokozi angezaliwa, na nyota mpya ikaonekana (ona 3 Nefi 1:19, 21). Kila kitu Bwana alichotolea unabii kupitia Samweli kuhusu kuzaliwa kwa Mwokozi kilitimizwa kama vile Bwana alivyosema kingekuwa.

Kuja kwa Mwokozi ulimwenguni haraka kuliokoa wale waumini kutokana na mauti. Lakini siyo tu kuliwaokoa wao pekee yao. Yesu Kristo alikuja kutuokoa sisi sote kutokana na dhambi na mauti, kutupa nguvu nyakati za shida, na kutuletea tumaini na shangwe kupitia Upatanisho Wake. Huu umekuwa ndiyo ujumbe mkuu wa kila nabii “ambaye [ame] toa unabii tangu kuanza kwa ulimwengu” (Mosia 13:33). Manabii hutuongoza kwa Mwokozi, ambaye ni “njia, kweli, na uzima” (Yohana 14:6).

Nabii Hutangaza Ukweli

Mara ya kwanza niliposoma Kitabu cha Mormoni nikiwa shule ya upili, mafundisho kutoka kwa Samweli Mlamani yalionekana ya kipekee kwangu. Yeye aliwaambia Wanefi kwamba kama wataendelea kuahirisha toba yao wakati ungefika ambao ingekuwa “wamechelewa milele.” Yeye alisema, “Kwani mmetafuta siku zote za maisha yenu yale ambayo hamwezi kuyapata; … mmetafuta furaha kwa kufanya uovu,” kitu ambacho ni kinyume cha asili ya Baba yetu wa Mbinguni (Helamani 13:38).

Katika siku yetu, Rais Nelson vile vile amefundisha:

“Wakati ulimwengu unasisitiza kwamba nguvu, mali, umaarufu na starehe za kimwili ndizo ziletazo furaha, hazileti! Haziwezi! …

“Ukweli ni kwamba ni ya kuchosha zaidi kutafuta furaha mahali ambapo huwezi kamwe kuipata! … Yesu Kristo … , na ni Yeye pekee, [aliye] na nguvu ya kukuinua juu ya nguvu za kudidimiza za ulimwengu huu.”

Baadhi ya Wanefi walichagua kumsikiliza na kuamini maneno ya Samweli; wengine wengi hawakufanya hivyo (ona Helamani 16: 1–8). Katika njia nyingi, leo siyo tofauti sana.

Je, wewe utachagua nini? Je, wewe utamsikiliza nabii?

Rais Nelson amefundisha:

“[Manabii, waonaji, na wafunuzi] yawezekana siyo siku zote wakawaambia watu mambo yale wanayotaka kusikia. Manabii ni nadra sana kupendwa na watu wengi. Lakini sisi siku zote tunafundisha ukweli!”

Unapomsikiliza nabii na kutendea kazi maneno yake, utaona kwamba mwongozo wake wa kinabii unakulinda, unakubariki, na kukusaidia katika maisha yako yote.