Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Unaogopa Toba?
Septemba 2024


Je, Unaogopa Toba?

Kulingana na Rais Russell M. Nelson, hapa kuna sababu wewe hupaswi kuogopa.

Je, wewe unaogopa nini? Bembea? Darasa la hisabati? Kujaribu kumwelewa Isaya?

Je, Kuhusu toba? Kama wazo la kutubu linakufanya wewe utake kujificha chini ya maficho au kula chokoleti nyingi sana, makala hii ni kwa ajili yako.

“Tafadhali usiogope au kuchelewa kutubu,” Rais Russell M. Nelson alisema. Na kwa sababu nzuri. Hapa kuna mambo machache ambayo toba ni na siyo, kulingana na Rais Nelson.

watu vijana mbalimbali

Vielelezo na Corey Egbert

mvulana akiwa na kalenda kubwa
msichana na mvulana wakiruka kwa shangwe
msichana ameshika mchoro wenye umbo la moyo
watu wakitembea kuelekea nyumba ya mkutano
mvulana akitembea na Yesu Kristo

Kubali Zawadi Kamilifu ya Mungu

Basi, uko tayari kumtumaini Mwokozi ili kushinda woga wako wa toba? Hautajutia.

Rais Nelson anasema: “Kwa sababu ulimwengu ulihitaji kuokolewa, na kwa sababu wewe na mimi tunahitaji kuokolewa, [Baba wa Mbinguni] alituletea Mwokozi.

“… Acha tukubali zawadi ya Mungu iliyo kamilifu na yenye thamani. Acha tutue mizigo na dhambi zetu miguuni pa Mwokozi na tufurahie shangwe ambayo huja kutokana na toba na badiliko.”