Sauti za Vijana
Ugonjwa Wangu wa Kutotaka Kula dhidi ya. Utambulisho Wangu wa Kweli
Kwa muda mrefu nilipambana na ugonjwa wa kutotaka kula unaoitwa anorexia nervosa, unapunguza kula kidogo kidogo na kuhofia kuhusu kuongezeka uzito. Unakuathiri kiakili—unaanza kuhisi hatia ya kula na huelewi mahitaji ya mwili wako. Haikusaidia kwamba kwa mwendelezo niliona viwango visivyo vya uhalisia mtandaoni au shuleni, nikaanza kujilinganisha mimi mwenyewe na familia yangu na wengine wanaonizunguka.
Ugonjwa wangu wa kutotaka kula hakika ulikuwa ukielezea kitu nilichokificha. Lakini mama yangu alitambua mabadiliko katika tabia yangu ya ulaji. Alikaa nami chini na kunipa muda wa kutosha kadiri nilivyohitaji ili nimwambie kinachoendelea. Kulikuwa na machozi mengi, lakini nafikiri Roho alimwongoza kujua kwamba nilihitaji msaada. Kwa pamoja, tulitengeneza mpango na kidogo kidogo tulianza kuufanyika kazi.
Wakati huo, mimi pia niliamua kupata baraka zangu za kipatriaki. Nilitaka kujua maisha yangu yangekuwaje nje ya kiza hiki ambacho nilikuwa ninakipitia. Nikaja kumuuliza Mungu,”Mimi ni nani?” “Je, Unanipenda?,” na “Kwa nini niko hapa?” Kitu cha kwanza Mungu alichoniambia kilikuwa ni jibu la maswali hayo. Baraka yangu hunisaidia kujifunza kuhusu utambulisho wangu wa kweli na kile Mungu alichokiweka kwa ajili yangu. Wakati wowote ninapoisoma, ninahisi upendo wa Mwokozi kwangu na kukumbuka kile ninachoweza kuwa pamoja Naye.
Hata kwa usaidizi wa baraka yangu ya kipatriaki, familia yangu, Baba yangu wa Mbinguni na Mwokozi wangu, ilinichukua muda mrefu kuchakata hisia nilizokuwanazo kuhusu mwili wangu. Bado ni vigumu wakati mwingine kujikubali mimi mwenyewe kwa jinsi nilivyo na kwa njia ninayoonekana. Kwa sababu ya nyakati zangu za kiza, ninaanza kushukuru ukuaji na nuru ambayo inakuja kutokana na kutambua utambulisho wangu wa kweli. Mimi ni binti wa Baba wa Mbinguni. Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo. Wananiangalia kwa upendo na kwa kunitia moyo, na hiyo ni muhimu zaidi kuliko maoni ya mtu mwingine yeyote yule.
Annalise B., umri miaka 17, Georgia, Marekani
Anafurahia kufanya kazi yake ya ukufunzi hospitalini na kutengeneza sanaa na muziki ili kumpa heshima Mungu na viumbe Wake.