Kupata—na Kutoa—Msaada wa Afya ya Akili
Linapokuja suala la afya ya akili, unaweza kuomba msaada na kutoa msaada kwa wengine pia.
Ni nini unapaswa kufanya wakati unapokuwa unahisi huzuni, kukatishwa tamaa, wasiwasi, mwenye hofu, au msongo wa mawazo?
Ungeweza kutegemea jibu kuwa kitu kama: Ishi injili. Sali. Soma maandiko. Pokea Sakramenti. Na kuendelea kufanya vitu kama hivyo ni vyema na muhimu na vinatatua (na kuzuia) matatizo mengi sana. Lakini baadhi ya matatizo yanahitaji juhudi za ziada.
Bila shaka, kila mtu huisi wasiwasi au huzuni wakati fulani. Hiyo ni sehemu ya maisha. Kuna njia nyingi za kiafya zenye kuendana na mambo haya. Lakini kama wasiwasi au msongo wa mawazo ni mkali sana au ni wa muda mrefu ambao unaingilia maisha yako na unakuzuia kumhisi Roho, basi unaweza kuwa kwenye hatua ambayo si ya uwezekano wa kutegemewa kuwa bora pasipo usaidizi wa ziada.
Afya ya akili ni afya ya kimwili (ona Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo kwa ajili ya Kufanya Chaguzi [2022], 29). Kemikali katika ubongo wetu hurekebisha hisia zetu, na ubongo ni sehemu ya mwili. Mtu yeyote anayesema msongo wa mawazo au wasiwasi “vyote viko katika kichwa chako” yuko sahihi tu katika maana halisi: kichwani mwako, kwa kweli, ndiko ubongo wako unakopatikana. Lakini matatizo haya ni ya kufikirika zaidi kuliko mguu uliovunjika au ugonjwa wa kidole tumbo.
Kupata Msaada
Kitabu cha Mormoni kinasema Wanefi walibarikiwa kwa kuwa na “mimea na mizizi mingi ya kiwango bora ambayo Mungu alikuwa ameitayarisha ili kutatua chanzo cha maradhi mengi” (Alma 46:40). Leo, tunaweza kuita vitu hivi dawa.
Leo, Mungu ametayarisha njia nyingi zaidi za kupambana na magonjwa na majeraha, ikijumuisha maumivu ya akili na kihisia. Sasa tunayo matibabu ambayo Wanefi—na mababu zetu, kuhusu jambo hilo hilo—kwao ilikuwa ni ndoto tu. Tunaishi katika enzi za miujiza! Na Baba wa Mbinguni anataka
Hiyo haimaanishi kwamba kila mtu anayepambana na msongo wa mawazo au wasiwasi anahitaji dawa au matibabu. Kila mtu ni wa tofauti. Lakini bila ya kujali hali yako ilivyo, kitu kimoja ni cha uhakika: Hakuna sababu ya kuteseka peke yako. Baba wa Mbinguni anayo shauku ya kukusaidia.
Baba yako wa Mbinguni anajua kile kitakachokusaidia wewe. Iwe mapambano yako yanaweza kutatuliwa kwa sala na imani, au iwe unahitaji pia kutafuta baraka Zake kupitia mchanganyiko wa dawa, matibabu, wazazi, marafiki, maaskofu, viongozi wa vijana, walimu, hewa safi, na mazoezi ili kukupitisha kwenye nyakati hizi ngumu, omba usaidizi Wake. Usihofu kupita kiasi kuhusu jinsi wengine walio na matatizo sawa na yako waliyatatuaje. Baba wa Mbinguni atakusaidia kupata suluhisho linalotosha kutatua hali yako.
Kuwa Mwenye Msaada
Injili ni juu ya kuwasaidia wengine, tukiakisi njia ambazo Mwokozi alitusaidia sisi kupitia Upatanisho Wake. Siku zote unapaswa kujaribu “kuwafikia wale wanaojisikia wapweke, wametengwa, au hawana msaada. Wasaidie wausikie upendo wa Baba wa Mbinguni kupitia kwako” (Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo kwa ajili ya Kufanya Chaguzi, 12). Yawezekana usiwe daktari au mtaalamu wa matibabu, lakini wewe ni mwanafunzi wa Yesu Kristo, na wanafunzi wa Kristo “wanaomboleza na wale wanaoomboleza; ndiyo, na kuwafariji wale wanaohitaji kufarijiwa” (Mosia 18:9).
Moja ya mambo muhimu unayoweza kufanya wakati mmoja wa uwapendao anapambana na msongo wa mawazo, wasiwasi, au matatizo mengine ya afya ya akili ni kumsikiliza.
Mara nyingi, mtu anayepambana na afya ya kihisia anachotaka tu kutoka kwako ni kumwonea huruma na kushiriki upendo wako. Hawategemei wewe kuwa na majibu ya kimuujiza ambayo yatatatua kila kitu. Yawezekana wanahitaji njia tu ya kutolea yaliyo ndani mwao. Wanahitaji mtu wa kuwa pamoja nao, kuwasikiliza, na kuonyesha huruma- kusema, ‘Nakubaliana na wewe, kitu unachopitia kinaonekana kuwa kibaya sana. Pole sana. Natamani ningeweza kukitatua. Tafadhali niambie jinsi ninaweza kusaidia.”
Na Kumbuka …
Iwe wewe ndiye unayetoa ,saada au mwenye kupokea msaada, kumbuka kwamba kuna baadhi ya mambo ni Mungu pekee ndiye anaweza kufanya. Mwache Yeye afanye. Kwa sasa, fanya kile wewe unachoweza ili kujijali mwenyewe na watu wanaokuzunguka.