2018
Somo la Kustaajabisha
April 2018


Somo la Kustaajabisha

“Nita … wafungulieni madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka” (Malaki 3:10).

An Amazing Lesson

Nilipokuwa nikikua huko Guatemala, familia yangu ilimiliki kiwanda kilichotengeneza sare za timu za michezo.

Baba yangu alitaka watoto katika familia yetu kujifunza kufanya kazi kwa bidii. Tulimsaidia kiwandani. Niliingia matatizoni mara nyingi nilipokuwa mdogo. Daima nilionekana mwenye kuvunja vitu! Lakini nilipokuwa mkubwa, baba yangu aliniacha niangalie mashine za kufuma.

Baba yangu alitulipa kwa kazi tuliyofanya. Kisha angeuliza, “Utakwenda kufanyia nini pesa zako?” Nilijua lipi lilikuwa jibu sahihi: “Kulipa zaka yangu na kuweka akiba kwa ajili ya misheni yangu.”

Nilipokuwa na miaka 13, biashara yetu ilipoteza pesa nyingi sana. Ilibidi tuondoe vyerehani vyetu vingi. Badala ya kuwa na wafanyakazi mia mbili, tulikuwa na wachache kuliko watano. Walifanya kazi katika gereji yetu nyumbani.

Nilikuwa daima nikilipa zaka yangu, lakini sikuwahi kuelewa hasa ilikuwa muhimu kiasi gani. Ndipo nilipojifunza somo la kustaajabisha. Jumamosi moja asubuhi niliwasikia wazazi wangu wakiongea pole pole. Baba yangu alimwambia mama yangu kwamba kulikuwa na pesa ya kutosha aidha kulipa zaka au kununua chakula. Hakukuwa na kiasi cha kutosha kufanya vyote. Nilipata hofu. Je, baba yangu angefanya nini?

Jumapili nilimuona baba yangu akipeleka bahasha kwa rais wetu wa tawi. Alichagua kulipa zaka! Nilifurahi kwamba alifanya hivyo, lakini pia nilikuwa na hofu. Je, tutakula nini?

Asubuhi iliyofuata watu fulani waligonga mlangoni kwetu. Walimwambia baba yangu kwamba walihitaji sare mara moja. Kwa kawaida watu walitulipa baada ya oda kumalizika. Lakini watu hawa walimlipa baba yangu siku ile, hata kabla hatujashona sare!

Katika mwisho wa wiki moja, nilijifunza somo zuri ambalo limedumu nami maisha yote. Sheria ya zaka hutusaidia kujenga imani yetu na kuonyesha shukrani yetu kwa Baba wa Mbinguni. Kulipa zaka ni baraka