Kwenye Hoja
Je, ni kwa nini Mungu huruhusu vita?
Vita imekuwa sehemu ya hadithi ya mwanadamu katika dunia hii tangu karibu mwanzo. Lakini Bwana, Mfalme wa Amani, hataki sisi tuanzishe vita sisi kwa sisi. Anatokwa machozi wakati watu wanapochagua kutopendana na “hawana upendo, na … wanaichukia damu yao wenyewe” (Musa 7:33), wameijaza dunia dhuluma (ona Mwanzo 6:11–13). Wale ambao uovu wao huleta vita duniani watahukumiwa kwa matendo yao.
Bwana amewaamuru watu Wake ku “kataa vita na kutangaza amani” (M&M 98:16). Hata hivyo, wakati mataifa yanaponyanyua silaha dhidi mmoja na mwingine, Bwana pia amesema kwamba sisi wakati mwingine tunahesabiwa haki katika kutetea familia zetu, mataifa, na uhuru dhidi ya maangamizo, ubabe na uonevu (ona Alma 43:47; Alma 46:12–13; M&M 134:11). Na Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaotumikia katika majeshi ya mataifa yao wanaunga mkono kanuni ya “kuwa chini ya wafalme, marais, watawala, na waamuzi” (Makala ya Imani 1:12).