Nini, Kwa nini, na Jinsi gani: Uainishaji wa Urejesho
April 2018
Nini, Kwa nini, na Jinsi gani: Uainishaji wa Urejesho
Na Faith Sutherlin Blackhurst
Magazeti ya Kanisa
Kufundisha injili, utahitajika kuweza kuelezea ukengeufu ni nini, vipindi vya mwongozo wa Mungu, na Urejesho. Chati hii inaweza kusaidia.
Tuseme uko kwenye safari ya wiki nzima pwani pamoja na familia ya rafiki yako. Mmekuwa na wakati mzuri, lakini unaanza kuikumbuka familia yako mwenyewe. Kisha baba yako anakutumia ujumbe mfupi kuona mambo yanaendaje—ndicho hasa ulichohitaji kuhisi unapendwa na kukumbukwa.
Maisha Ulimwenguni kwa kiasi kidogo ni kama hivyo. Mungu hatutumii ujumbe mfupi, lakini tupo mbali na nyumbani kwetu mbinguni, hivyo njia moja ambayo Baba wa Mbinguni huwasilisha upendo Wake kwetu ni kwa kuwatuma manabii.
Kipindi cha Mwongozo wa Mungu
Manabii huongoza kile kinachoitwa vipindi vya mwongozo wa Mungu, vipindi vya nyakati ambapo (1) Mungu anakuwa na angalau kiongozi mmoja wa ukuhani aliyepewa mamlaka duniani na (2) kiongozi huyu, nabii, hujifunza kuhusu mpango wa wokovu moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Nabii kisha hufundisha, au hutoa, injili kwa watu.
Shukrani kwa maandiko, tunajua kuhusu vipindi vingi vya mwongozo wa Mungu. Baadhi ya vile muhimu ilikuwa ni cha Adamu, Henoko, Nuhu, Ibrahamu, Musa, Yesu Kristo na Joseph Smith. Bwana alianzisha kipindi cha mwongozo wa Mungu kupitia kila mmoja wa manabii hawa.
Ukengeufu
Ukengeufu=uovu. Wakati mtu binafsi au kikundi wanapogeuka kutoka kwenye ukweli wa injili ya Yesu Kristo, wanawakataa manabii, na kuanguka katika dhambi, wanakuwa katika ukengeufu.
Urejesho
Urejesho ni tendo la kurudisha kitu katika hali yake halisi. Siyo kutengeneza upya, ambako ni kubadilisha kitu kilichopo na kutengeneza kitu kipya. Kwa mfano, kama ukitaka kurejesha nyumba ya zamani, utaijenga upya kwa mpangilio ule ule halisi iliyokuwa nao. Unaweza kuhitaji kuongeza sehemu mpya ya mekoni, lakini hapo utakuwa unabadilisha nyumba, siyo kuirejesha.
Injili ya Yesu Kristo ilihitajika kurejeshwa kwa sababu ilipotea wakati wa Ukengeufu Mkuu. Watu walikuwa wameishi kwa karne nyingi bila Kanisa la kweli. Hivyo Bwana alirejesha Kanisa Lake na injili kupitia Joseph Smith, kama vile manabii wa kale walivyotoa unabii (ona Isaya 2:1–3; 29:13–14; Matendo ya Mitume 3:19–21; Ufunuo 14:6–7; 2 Nefi 3:3–15).
Injili ya kweli ya Yesu Kristo iko hapa daima—kwa hivyo wewe utakaa nayo daima? Japokuwa ulimwengu unakua mwovu zaidi na zaidi, Kanisa la Yesu Kristo litabaki hadi mwisho.
Una uchaguzi wa kufanya—uchaguzi ule ule ambao umewapata wanadamu tangu mwanzo wa nyakati: je, utamfuata nabii? Ukimfuata nabii, utabarikiwa na kuwa na Roho ili kukuongoza.