2018
Kuja Kumjua Mwokozi
April 2018


Kuja Kumjua Mwokozi

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Unapojifunza kuhusu Yesu Kristo, unaalika amani na uwepo Wake katika maisha yako.

Christ praying

Utondoti wa kina kutoka Wako Wapi wale Kenda, na Liz Lemon Swindle

Fikiria kusoma kila kitu kumhusu Mwokozi katika maandiko—Biblia Takatifu, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, Lulu ya Thamani Kuu. Zungumza kuhusu muda mwingi na kazi! Lakini mnamo Januari 2017, Rais Russell M. Nelson, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alitoa changamoto ya kufanya hilo tu—kujifunza kila kitu ambacho Yesu alisema na kufanya katika vitabu vya kanisa. Rais Nelson alisema kwamba kumaliza mradi huu kulimfanya “mtu tofauti.” Siyo tu kwamba alijifunza zaidi kumhusu Yesu Kristo lakini pia alihisi upendo mpya Kwake.1

Wewe pia unaweza kusogea karibu na Kristo unapojifunza kumhusu Yeye. Kujifunza maisha Yake na madhumuni Yake hualika amani Yake katika maisha yako na hukusaidia kuja kumjua Yeye na Baba wa Mbinguni. Angalia jinsi vijana hawa walivyojibu maswali mawili: (1) Je, ni hadithi ipi ya maandiko unayoipenda zaidi kumhusu Mwokozi na kwa nini? (2) Na ni kwa jinsi gani kujifunza kwako injili kumekuletea amani?

Ninaipenda hadithi ya wakoma 10 kwa sababu Kristo alionyesha upendo mkubwa kwa mkoma aliyemshukuru. Alisema, “Imani yako imekuponya” (Luka 17:19; ona mstari 11–19). Ninapenda ukarimu halisi ambao Yeye alimuonyesha kila mmoja.

Kwa sababu ya majanga ya hivi karibuni katika shule yangu, kila mmoja shuleni anahitaji amani na faraja kubwa. Nimepata nguvu na amani kupitia kujifunza kwangu katika seminari. Walimu wa seminari hufanya maandiko na injili kuwa ya binafsi kwa kila mmoja. Ni vizuri sana kuona tofauti ya darasa la seminari ikilinganishwa na darasa la kawaida. Kuna hisia tofauti inayoleta amani katika darasa la seminari.

Gabriel S., umri miaka 16, Colorado, Marekani

Hadithi ya Alma kuhusu imani na neno la Mungu (ona Alma 32:18–43) imenifundisha kwamba tunapopanda upendo, tunapokea upendo. Kama Alma anavyowaelezea Wazoramu, imani ni kama mbegu. Ni kusadiki kwamba jambo fulani ni la kweli bila hasa kuwepo pale kuliona. Imani hukua wakati mtu anapokuwa na hamu ya kuamini na kusikia neno la Mungu. Haya yote yamenifanya kuwa mtulivu, kuimarisha moyo wangu, na kupata ushuhuda kwamba Baba wa Mbinguni ananiona kwa macho ya upendo na rehema.

Ninaposoma maandiko kila siku, Ninaelewa zaidi upendo ambao Mwokozi anao kwa kila mmoja wetu. Ufahamu huu hunisaidia kuelezea kwa marafiki zangu shuleni kwamba hawako peke yao wanapokuwa na matatizo kwa sababu kuna Mungu anayetupenda.

Maria D., umri miaka 17, Guadalajara, Uhispania

Christ with children

Utondoti wa kina kutoka Kristo na Watoto wa Kitabu cha Mormoni, na Del Parson

Ninapenda 3 Nefi 17 wakati Mwokozi anatembelea Amerika na kuwaalika watoto kuja Kwake. Anakaa nao na anatumia muda kuwa pamoja nao mmoja mmoja. Hiyo ni hadithi ya kupendeza kwangu inayoonyesha Yesu Kristo ni nani na ana upendo kiasi gani kwa kila mmoja wetu. Ninaamini Yeye atakaa pia na kila mmoja wetu tunapohitaji msaada Wake.

Mwaka huu nilijipa changamoto ya kusoma ukurasa wa maandiko kila siku. Ninapokuwa nimefanya hivyo, nimekua kwa kitazamia kufanya hivyo kila siku. Nimejifunza mengi kutoka kwenye maneno na hadithi katika maandiko nilipojaribu kutumia muda kuyaelewa, na nimesogea karibu na Baba yangu wa Mbinguni na Mwokozi nilipojifunza kuwahusu Wao pia. Hiyo imeleta amani kubwa kwenye maisha yangu.

Anna C., umri miaka 17, Montana, Marekani

Ninapenda wakati Kristo anakuja Amerika, akiuliza kama kuna wagonjwa na wanaosumbuka miongoni mwao, na kisha anawaponya. Kisha anawabariki watoto wadogo. (Ona 3 Nefi 17) Nafikiria ni hadithi nzuri na yenye nguvu. Ninapenda watoto wadogo, na ninapenda watu wanapowapa upendo zaidi, kwa sababu watoto ni wasafi sana. Hadithi inanionyesha kina cha upendo wa Mwokozi kwa ajili yetu. Kwa kuwa aliwapenda watu huko nyuma kiasi cha kufanya kila kitu alichofanya, Anaweza kutupenda sisi pia leo.

Isaya 53:3 inasema Mwokozi ni “mtu wa huzuni nyingi, na ajuaye sikitiko.” Ninapofikiria kuhusu Upatanisho wa Kristo, Alichopitia kwa ajili yetu, na jinsi Ninavyoweza kusamehewa Ninapotubu dhambi zangu, Ninahisi amani hasa. Watu wengi katika Kitabu cha Mormoni—wana wa Mosia, Amoni, na Alma Mdogo—walikuwa na historia zisizo nzuri, lakini waliweza kusamehewa. Walimgeukia Kristo, wakatubu, na wakawa mifano mizuri ambayo kwayo tunaweza kujifunza leo. Inaleta faraja kwangu kujua Ninaweza kusamehewa pia.

Alina T., umri miaka 18, Oregon, Marekani

Hadithi yangu niipendayo zaidi katika maandiko kuhusu Yesu ni pale alipogeuza maji kuwa divai wakati wa harusi, aliposhawishiwa na mama Yake (ona John 2:1–11). Hadithi hii ninaipenda zaidi kwa sababu inaonyesha heshima ya Yesu kwa wanawake na hususani mama Yake. Hadithi hii huwahimiza watoto kuwaheshimu wazazi wao, si kwa nidhamu ya woga, bali kwa upendo mkubwa. Mfano wa Yesu Kristo ndicho kitu ambacho kila mtu anapaswa kujitahidia. Upendo Wake kwa mama Yake katu haukukoma, na wala upendo wetu kwa wazazi wetu haupaswi. Pia ni kifungu changu ninachokipenda zaidi kwa sababu muujiza Wake ni tendo la huduma, na sisi pia tunaweza kutengeneza miujiza kwa kuwasaidia wengine.

Hadithi hii na hadithi nyinginezo katika maandiko zimeniletea amani. Inaleta faraja kubwa kujua kwamba kama daima ninajaribu kujifunza juu ya Kristo na kufuata mafundisho Yake, siku moja ninaweza kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo.

Anne R., umri miaka 17, Victoria, Australia

Ninapenda hadithi ya Kristo wakati anatembea juu ya maji. Anatembea kuelekea chomboni ambamo Mitume wote wamo, na anamualika Petro kutembea juu ya maji. Petro ana imani mwanzoni na anaweza kutembea juu ya maji, lakini kisha anapoteza imani yake na anaanza kuzama. Kisha Kristo ananyoosha mkono Wake na kumshika (ona Mathayo 14:25–33). Hadithi inanivutia kwa sababu Kristo daima anaweka mikono Yake katika maisha yetu—anatulinda.

Kujifunza kwangu kunanisaidia kwa sababu ninajifunza maandiko yangu asubuhi na inafanya siku kuwa nzuri zaidi. Ninapoacha kusoma, siku yangu haiwi ya furaha—sijisikii vizuri. Ninaposoma maandiko yangu kila mara asubuhi, siku yangu inakuwa nzuri sana kwa sababu ninamualika Roho Mtakatifu kuwa nami katika siku hiyo.

James K., umri miaka 17, Alaska, Marekani

Christ and the rich young man

Utondoti kutoka kwa Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hoffmann

Ninapenda hadithi ya Kristo na kijana tajiri (ona Marko 10:17–22). Inanipa umaizi na mtazamo mkubwa kuhusu kumpa kipaumbele Mungu juu ya kila kitu. Kuambiwa kuuza kila mali ya ulimwengu uliyo nayo ingekuwa ombi gumu sana kwa kila mtu. Lakini nafikiri kwamba kuwa radhi kumuweka Mungu juu ya mali ni mojawapo ya vitu ambavyo kila mmoja wetu anapaswa kujifunza katika maisha. Upendo wa Yesu Kristo kwa ajili yetu usio na mipaka kweli ni wa kustaajabisha. Ni bora hasa zaidi ya kiasi cho chote cha pesa au mali tunazopata katika maisha haya.

Kusoma maandiko hunipa amani na faraja, vilevile hekima na uelewa mkubwa. Japokuwa Naweza daima nisijisikie kwa haraka nguvu ya kujifunza maandiko, ninajua kwamba kusoma maandiko hushawishi maisha yangu katika njia chanya na hunisaidia kumhisi Roho na kutambua ushawishi Wake.

Yuzhen C., umri miaka 19, Taichung, Taiwan

woman touching the hem

Utondoti wa kina kutoka Mwanamke Anagusa Pindo la Vazi la Yesu, na Heidi Daynes Darley

Wakati Kristo akiwa njiani akienda kumwona binti mdogo anayekufa, mwanamke mwenye tatizo la damu anagusa tu vazi Lake na anaponywa. Kristo anageuka na anaongea naye baada ya kugundua kwamba amemgusa (ona Luka 8:43–48). Licha ya kwenda kumsaidia mtu mwingine, Kristo alitoa muda kwa ajili yake pia. Kristo hutupatia muda sote pia.

Ratiba ya maisha yangu hakika imebana, kukimbia kwenda shuleni au madarasa ya bale au kazi zingine. Wakati wa hayo yote, sipati muda wa kuwa peke yangu au kuhisi amani. Ninaposoma maandiko yangu au kuomba, ninahisi amani. Ni vizuri kuhisi hivyo na kuwa na mapumziko kutoka kwenye wendawazimu huu. Katika nyakati hizo za amani, Ninakua karibu na Mwokozi na kukua katika injili.

Zoe B., umri miaka 17, Utah, Amerika

Muhtasari

  1. Ona Russel M. Nelson, “Manabii, Uongozi, na Sheria Takatifu” (ibada ndogo ya ulimwengu wote kwa vijana wakubwa, Jan. 8, 2017), broadcasts.lds.org; “Kuleta Nguvu ya Yesu Kristo katika Maisha Yetu,” Apr. 2017 mkutano mkuu; “Jifunze Maneno ya Mwokozi,” Liahona, Jan. 2018, 56–59.