Taswira za Imani
Rakotomalala Alphonse
Sarodroa, Madagaska
Wakati Rakotomalala alipovutiwa na injili, kanisa la karibu lilikuwa huko Antsirabe, mji ulioko maili 30 (km 50) kutoka kijiji chake huko Sarodroa. Rakotomalala na rafiki yake walitafuta njia za kusafiri kila Jumapili.
Leo, Sarodroa ina jumba dogo la mkutano ambapo zaidi ya waumini 100 wanahudhuria kila Jumapili. Rakotomalala ameona kijiji chake kikiikumbatia injili. Wamisionari wanne wameshatumikia wakitokea Sarodroa na Kanisa linaendelea kukua.
Cody Bell, mpiga picha
Wakati babu yangu alipokuwa mgonjwa, Nilisafiri kwenda Antsirabe kumuuguza. Wamisionari walitembelea nyumbani kwake mara kadhaa. Mimi na babu hatukuwa waumini wa Kanisa, lakini babu alipenda kukutana na wamisionari. Usiku mmoja, walimpa babu baraka, na baada ya jioni ya familia nyumbani, walitupatia Kitabu cha Mormoni.
“Tafadhali someni kitabu hiki na mwombeni Mungu ili kujua kama ni cha kweli,” walisema.
Niliporudi Sarodroa, sikutaka kusoma Kitabu cha Mormoni kwa sababu nilidhani si cha kweli. Kisha, siku moja niliugua sana kiasi kwamba niliganda ndani ya nyumba yangu kwa siku kadhaa. Nilipotafuta kitu cha kufanya, nilipata Kitabu cha Mormoni na kuanza kukisoma.
Baadaye, Nilirudi Antsirable na kukutana na wamisionari. Walinifundisha zaidi kuhusu Kitabu cha Mormoni na kuhusu Nabii Joseph Smith. Niliwaambia kwamba hatukuhitaji manabii na kwamba hakukuwa na nabii leo. Wamisionari walinitaka niombe kwa Mungu na kumuuliza kama kuna nabii sasa. Waliahidi kwamba Mungu angenijibu. Niliomba na kuhisi kwamba kile wamisionari walichosema kilikuwa kweli.
Nilitaka kuhudhuria kanisani, lakini sikuwa na pesa ya kupanda basi. Niliongea na rafiki yangu, Razafindravaonasolo, na alisema tungeweza kutumia baiskeli yangu. Tuliendesha baiskeli kwa saa mbili kutoka Sarodroa mpaka Antsirable kila Jumapili. Nilipochoka kupiga pedali, ningekaa kiti cha nyuma na rafiki yangu angeanza kupiga pedali. Alipochoka, tungebadilishana tena.
Hatimaye, Mimi na familia ya Razafindravaonasolo tulijiunga na Kanisa. Tulihudhuria kanisani huko Antsirable mpaka tawi lilipofunguliwa Sarodroa. Tulikuwa na furaha sana tulipoweza kuhudhuria kanisani katika kijiji chetu wenyewe!
Baba yake Razafindravaonasolo aliitwa kama rais wa tawi. Siku moja alikutana nami na kunihimiza nijiandae kwenda misheni. Sikudhani kama ningeweza kutumikia, lakini alinihakikishia kwamba ningeweza. Nilikubali wito wa kutumikia katika misheni ya Madagascar Antananarivo. Nimeoa sasa na nina watoto wawili. Ninashukuru kwa ajili ya familia yangu, na nimekuwa na uzoefu mwingi Ninaoweza kuelezea ambao umenisaidia kujua kwamba Kanisa hili ni la Kweli.