Mpaka Tutakapokutana Tena
Uhalisi wa Ufufuko
Kutoka katika hotuba iliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa Aprili 2014.
Yesu Kristo kwa kweli ndilo jina pekee au njia ambayo kwayo wokovu unaweza kumjia mwanadamu.
Fikiria kwa muda umuhimu wa Ufufuko katika kuamua mara moja na kwa mara zote utambulisho wa kweli wa Yesu wa Nazareti na mashindano makubwa ya kifalsafa na maswali ya maisha. Kama kweli kabisa Yesu alifufuka, inafuata umuhimu kwamba Yeye ni kiumbe kitakatifu. Hakuna kiumbe chenye mwili wenye kufa kilicho na nguvu ndani yake ya kurudia uhai tena baada ya kufa. Kwa sababu Yeye alifufuka, Yesu hawezi kuwa alikuwa tu seremala, mwalimu, rabi, au nabii. Kwa sababu Yeye alifufuka, Yesu lazima alikuwa Mungu, hata Mwana wa Pekee wa Baba.
Kwa hivyo, kile Alichofundisha ni kweli; Mungu hawezi kudanganya.
Kwa hivyo, Yeye alikuwa Muumbaji wa dunia, kama Yeye alivyosema.
Kwa hivyo, mbingu na jehanamu ni hakika, kama alivyofundisha.
Kwa hivyo, kuna ulimwengu wa roho, ambao Yeye aliutembelea baada ya kifo Chake.
Kwa hivyo, Atakuja tena, kama malaika walivyosema, na “kutawala mwenyewe juu ya dunia” [Makala ya Imani 1:10].
Kwa hivyo, kuna ufufuo na hukumu ya mwisho kwa wote.
Kutokana na ukweli juu ya Ufufuko wa Kristo, shaka kuhusu mwenye kudura, mwenye kujua yote, na ukarimu wa Mungu Baba—aliyemtoa Mwanawe wa Pekee kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu—hazina msingi. Shaka kuhusu maana na madhumuni ya maisha hazina msingi. Yesu Kristo kwa kweli ndilo jina pekee au njia ambayo kwayo wokovu unaweza kumjia mwanadamu. Neema ya Kristo ni halisi, ikiwezesha vyote msamaha na kusafishwa kwa mtenda dhambi anayetubu. Imani kwa kweli ni zaidi ya fikra au uvumbuzi wa kisaikolojia. Kuna ukweli wa mwisho na kwa ulimwengu wote, na kuna lengo na viwango vya kimaadili visivyobadilika, kama ilivyofundishwa na Yeye.
Kufuatia uhakika wa Ufufuko wa Kristo, toba kwa ukiukaji wa sheria na amri Zake vyote inawezekana na ni muhimu. Miujiza ya Mwokozi ilikuwa halisi, kama ilivyo ahadi Yake kwa wanafunzi Wake kwamba nao wafanye vivyo hivyo na hata kazi kuu zaidi. Ukuhani Wake ni nguvu muhimu halisi ambayo “uhuidumia injili na kushikilia ufunguo wa siri za ufalme, hata ufunguo wa ufahamu wa Mungu. Kwa hiyo, katika ibada hizo, nguvu za uchamungu hujidhihirisha” [M&M 84:19–20]. Kufuatia uhalisi wa Ufufuko wa Kristo, kifo siyo mwisho wetu, na baada ya “ngozi [yetu], kuharibiwa hivi, Lakini, katika miili [yetu] [tu]tamwona Mungu” [Ayubu 19:26].