2018
Hapa Ndipo Mahali
April 2018


Hapa Ndipo Mahali

Simeon Nnah

Aba, Naijeria

man standing in the temple

Kielelezo na Allen Garns

Baba yangu, Mkristo mcha Mungu, alinifundisha kuwa na imani katika Yesu Kristo. Imani hiyo ilinisaidia kunusurika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka-mitatu vya Nigeria mnamo mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati nilipokuwa jeshini. Baadaye, hata hivyo, nilitatizika na kuacha kuhudhuria kanisa.

Nilipokuja Marekani mnamo 1981 kupata elimu, Nilihisi kwamba nilimuhitaji Mungu katika maisha yangu. Kwa miaka miwili nilihudhuria makanisa tofauti katika Boston, Massachusetts, lakini hakuna hata moja lililonivutia. Sikuhisi Roho, hivyo niliacha kutafuta.

Si muda mrefu baada ya mke wangu, Mabel, kuungana nami kutoka Nigeria mnamo 1984, Nilianza kuwa na tamaa kubwa ya kusogea tena karibu na Mungu na kuwa muumini wa kanisa. Rafiki aliyekuwa ametutembelea kutoka Nigeria hakujua kama nilikuwa natafuta kanisa, lakini aliniambia kuhusu kanisa alilokuwa amesikia ambalo lilikuwa na kitabu kilichoitwa Kitabu cha Mormoni.

Baada ya hapo, mimi niliendelea kutafuta makanisa. Nilipata kanisa lililoitwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho Neno mtakatifu lilivuta hisia zangu. Sikujua kama kulikuwa na kanisa lenye waumini walioitwa watakatifu. Jumapili ile niliamua kwenda kuangalia.

Katika mkutano wa sakramenti niliohudhuria, mkutano uliimba nyimbo za kanisa katika njia ya unyenyekevu, makuhani walibariki mkate na maji, na ibada iliendeshwa kwa mpangilio na kwa unyenyekevu. Baada ya hapo, nilipokuwa nikitembea kuelekea ukumbini na kutafakari ile ibada, nilisikia jina langu.

“Simeon,” sauti ya Roho ilisema, “hapa ndipo mahali.”

Katika hatua ile, wamisionari wawili walinikaribia. Walijitambulisha wenyewe na Kitabu cha Mormoni. Niliwatazama na kusema, “sijui chochote kuhusu Kitabu cha Mormoni, lakini ninajua Biblia. Niko tayari.”

Walianza kunifundisha mpango wa wokovu. Kabla ya mwezi kwisha baadaye, nilibatizwa. Mke wangu alijiunga na Kanisa muda mfupi baadaye. Miaka michache baada ya hapo, tuliunganishwa katika Hekalu la Washington D.C. na watoto wetu watano waliunganishwa kwetu.

Ndani ya hekalu, mambo mengi yamekuwa yakifunuliwa kwangu, lakini maneno niliyosikia siku yangu ya kwanza kanisani yamekuwa yakithibitishwa kwangu mara nyingi kupitia ufunuo hekaluni: “Hapa ndipo mahali.” Matokeo ya kauli ile kutoka kwa Roho Mtakatifu daima imebadilisha maisha yangu na maisha ya mke wangu na watoto.