2023
Jiunge
Machi 2023


“Jiunge,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2023.

Jiunge

Rikuto I.,

16, Japani

Picha
mvulana

Picha na Sayaka Okubo

Jina langu ni Rikuto, na ninatoka Jiji la Matsudo, Japani.

Wakati wa shughuli ya jioni ya nyumbani, nilitumia app ya Family Tree ili kujifunza kuhusu mababu zangu walikuwa ni kina nani na maisha yao yalikuwa ya namna gani. Nilishangaa kujifunza kwamba mmoja wa mababu zangu alikuwa askari ambaye alikuwa anamlinda mfalme wa Japani ambaye aliishi zamani sana.

Mimi napenda kucheza soka, lakini kwa sababu mimi ni muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, sikutaka kucheza siku za Jumapili. Ilikuwa vigumu kwangu kumwambia kocha wangu kwamba nisingeweza kufanya mazoezi siku ya Jumapili, lakini nilipomwambia kuwa ninahudhuria kanisa, yeye bado aliniacha nijiunge na timu.

Kwa vile nilikosa mazoezi ya siku ya Jumapili, wana timu wenzangu daima hawakuamini ujuzi wangu. Nilisali ili niweze kufokasi na kucheza vyema wakati wa mazoezi, kwa vile sikuwa na wakati mwingi wa mazoezi kama wenzagu wengine katika timu. Wakati mashindano ya mwisho yalipofika, nilialikwa kushiriki katika mchezo. Ninajua Mungu alinisaidia kufikia lengo hilo.

Chapisha