2023
Mwokozi Anajua Jinsi ya Kunisaidia Mimi Kupitia Saratani
Machi 2023


“Mwokozi Anajua Jinsi ya Kunisaidia Mimi Kupitia Saratani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2023.

Nayaweza Mambo Yote katika Kristo

Vijana wanashiriki jinsi Kristo alivyowaimarisha wao kufanya mambo magumu (ona Wafilipi 4:13).

Mwokozi Anajua Jinsi ya Kunisaidia Mimi Kupitia Saratani

msichana

Maisha yangu yalikuwa ya kawaida kabisa mpaka majira ya baridi ya mwaka 2020. Nilikuwa mgonjwa wa kile tulifikiria yalikuwa ni maambukizi, kwa hiyo nilikunywa dawa za kuondoa maambukizi. Baadaye, nilianza kuhisi maumivu ya kichwa, kuchoka na kuzimia. Punde baadaye niliamka karibu saa 4 usiku nikifikiri ilikuwa asubuhi na kuanza kujiaanda kwenda shule.

Wakati dada yangu aliponiambia bado ni usiku, nilikimbilia kwenye chumba cha wazazi wangu katika hali ya kupagawa. Mama yangu aligusa kichwa changu na nilikuwa na joto la homa kali. Tulienda kwa daktari siku iliyofuata, ambaye alifanya vipimo vingi.

Usiku huo wazazi wangu walikuja chumbani kwangu, wakilia. Waliniambia kuwa nilikuwa na lukemia (saratani ya damu) na kwamba ilibidi twende hospitali kupata majibu zaidi. Nilikuwa katika chumba cha dharura usiku mzima na kuanza matibabu yangu ya tibakemikali siku chache tu baadaye.

Matitabu yangu yataendelea kwa mwaka mwingine mmoja au miwili, lakini nina nafuu kidogo. Nimekuwa nikihisi vizuri kidogo hivi karibuni na natumaini kwenda shuleni tena hivi karibuni. Ingawa, sio rahisi. Tibakemikali ina athari nyingi, ikijumuisha maradhi ya mifupa yanayoitwa uozo wa seli za mfupa ambayo yalifanya iwe vigumu kwangu kutembea.

msichana hospitalini

Licha ya haya yote—labda hata kwa sababu yake—nimesogea karibu zaidi na Baba yangu wa Mbinguni. Sasa nina uelewa wa kina juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Nilikuwa ninafikiria juu ya Upatanisho Wake kama kitu fulani unachokihitaji tu wakati unapofanya makosa. Hiyo ni sehemu yake, lakini kumtegemea Mwokozi pia ni kitu ambacho kimenisaidia kutohisi mpweke.

Yesu Kristo amejichukulia juu Yake Mwenyewe mateso yetu yote na dhambi zetu zote, ambayo inamaanisha Yeye anajua hasa jinsi ya kunisaidia ninapokabiliana na lukemia. Kwa kupitia jaribu lolote inaweza kuonekana kama kutengwa, lakini kupitia Upatanisho wa Kristo, tunaweza kupata faraja katika kujua kwamba Yeye hakika anaelewa kile tunachopitia.

Ruby H., Utah, Marekani