2023
Tayari Kuwa Mmisionari
Machi 2023


“Tayari Kuwa Mmisionari,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2023.

Tayari Kuwa Mmisionari

Ni kwa jinsi gani unajua kuwa umejiandaa kutumikia misheni?

Picha
wamisionari

Rais Russell M. Nelson ametukumbusha umuhimu wa kazi ya umisionari na amewahimiza wavulana na wasichana kujiandaa kutumikia misheni.1 Kuwa mmisionari kunahitaji kazi, lakini vile vile kuwa mmoja wao!

Maandalizi ya misheni wakati mwingine yanaweza kuonekana ya kuogofya kwa sababu inaonekana kama kuna vitu vingi sana vya kufanya:

“Ninahitaji kuweka akiba ya fedha.”

“Ninapaswa kujifunza Hubiri Injili Yangu.

“Ni kwa jinsi gani nitajipikia au kujifulia nguo mwenyewe?”

“Ninapaswa kupanga miadi na askofu wangu.”

“Je, mimi ninajiamini vya kutosha kushiriki injili?”

Mawazo haya na wasiwasi ni sawa. Hata hivyo, ni bora kufokasi katika dhumuni kuu la huduma yako.

Sababu Zako

Ni ya msaada kujiuliza mwenyewe: “Kwa nini ninataka kutumikia misheni?”

Labda unahisi kama ni wajibu wako. Labda umesisimka kuishi katika sehemu mpya au kujifunza lugha mpya. Pengine unataka kushiriki ushuhuda wako juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo au mafundisho juu ya familia za milele. Au unaamini, kama Rais Nelson vile alivyosema, kwamba “kila mmoja anastahili fursa ya kujua kuhusu injili ya urejesho ya Yesu Kristo.”2

Baadhi ya sababu za kutumikia misheni ni nzuri kuliko zingine, na kuna zaidi ya sababu moja nzuri ya kwenda misheni. Sababu zako zinapaswa hatimaye kukita katika upendo wako wa Bwana na injili Yake ya urejesho. Fikiria kuhusu sababu zako na kama zingekusaidia kumtumikia Bwana “kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu zako zote” (Mafundisho na Maagano 4:2). Na kama hauna shauku hiyo, unaweza kusali kwa Baba wa Mbinguni ili akusaidie kuipata.

Picha
dada mmisionari akitoa huduma

Ushuhuda Wako

“Je, ninao ushuhuda juu ya Urejesho wa injili ya Yesu Kristo? Na ninaamini kweli Yeye ameniita kutumikia misheni?”

Madhumuni ya mmisionari ni kuwaalika wengine waje kwa Kristo. Kama unawaalika watu kujifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake, ni muhimu kuwa na ushuhuda wako wewe mwenyewe.

Ushuhuda wako sio lazima uwe kamili; daima kutakuwa na nafasi ya kuukuza. Kile kilicho muhimu hasa ni msingi: Yesu Kristo. Unaweza kuja kumjua Yeye wewe mwenyewe kwa kujifunza maneno Yake katika maandiko, kusali kwa Baba wa Mbinguni katika jina Lake na kujitahidi kuishi kama Yeye.

Kuwa mmisionari mzuri haimaanishi wewe ni mzuri daima katika kuzungumza na watu au kukariri kila andiko (ingawaje daima unaweza kufanya kazi ya kuboresha ujuzi wako). Alimradi unayo matumaini katika Bwana, unaamini katika Yeye, na uko tayari kufanya kazi Yake, Yeye atakuza juhudi zako na kukusaidia kukufanya mmisionari mwenye tija.

Picha
wakina dada wamisionari

Endaumenti Yako ya Hekaluni

“Ninahisi niko tayari kwenda hekaluni?”

Kabla hujatumikia misheni, kuna uwezekano wa kupokea endaumenti yako katika hekalu kama bado utakuwa hujafanya hivyo.

Baraka za hekaluni ni “za msingi lakini mara nyingi ni kipengele kinachosahaulika katika maandalizi kwa ajili ya wito wa kazi hii.” Na “ustahili binafsi ni kigezo kimoja muhimu sana katika kupokea baraka za hekaluni.”3 Unapojiandaa na kuwa mwenye kustahili kwenda hekaluni na kufanya maagano matakatifu na Mungu, utakuwa pia unajiandaa mwenyewe kuwa mmisionari kwa ajili Yake (ona Mafundisho na Maagano 105:33; 109:22).

Hatimaye, unaweza kujiunga na darasa la maandalizi ya kwenda hekaluni. Lakini kwa sasa, unaweza kufanya mafunzo na maandalizi yako wewe mwenyewe. Rais Nelson amependekeza maandiko fulani na mada za injili unazoweza kujifunza kuhusu hekalu.4 Unaweza pia kujifunza zaidi katika temples.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
mmisionari wa huduma kwenye kompyuta

Mwenye kustahili na Mwenye Kujiandaa

Tena, kuna vipengele vingi vya maandalizi ya misheni. Ndiyo, wewe unapaswa kuweka akiba ya fedha, kujiweka imara katika afya ya kimwili na kujifunza ujuzi wa msingi kama vile kushona nguo kwa mkono au kupika. Unaweza pia kuwa na malengo hayo.

Lakini usikubali maelezo mengi yakuogopeshe. Maandalizi ya muhimu sana unayoweza kufanya ni aina ya yale ambayo yanakuruhusu kuwa chombo kinachostahili na kinachofaa katika mikono ya Bwana.

Kama unahisi kutofaa vya kutosha, wasiwasi, au kukosa uhakika kuhusu kutumikia, hiyo ni kawaida. Kumbuka tu kwamba Bwana anakutaka ufanikiwe! Unapokuwa unamtegemea Yeye na kufuata mwongozo wa Roho, Yeye atakusaidia kuwa mmisionari bora unayeweza kuwa.

Chapisha